Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Mfahamu Mzee Small.
Said Wangamba (Mzee Small) alizaliwa 1955 mkoani Lindi. Na baadae alihamia Dar mwaka 1970 ambapo alipata umaarufu kupitia uchekeshaji na uigizaji.
Alipewa jina la utani la Mzee Small kutokana na mwili wake kuwa mdogo. Alipata umaarufu kupitia baadhi ya kazi zake kama vile kama 'Hamsini Hamsini Mia' na 'Mjini Shule'.
Aliwahi kujiunga na vikundi mbalimbali vya sanaa vikiwemo Agizo Group, Muungano Culture Troupe, Shirika la Reli, Shirika la Wakala za Meli (Nasaco) na vingine kabla mwaka 1983 kwenda nchini Uingereza kwa maonyesho kadhaa ya sanaa.
Alifariki dunia Juni 8, 2014, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili amabapo alikuwa anapatiwa matibabu baada ya kuugua kiharusi kwa miaka miwili.
- TANZIA - Said Ngamba alias 'Mzee Small wa Ngamba' afariki dunia