Unamkumbukaje Alvaro Recoba

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Leo tunae [emoji117] Alvaro Recoba

Anaitwa Alvaro Alexander Recoba Rivero alizaliwa mwaka 1976 huko Montivedo Uruguay. Jina lake la utani lilikuwa "El Chino" likiwa na maana ya mchina, hii ni kutokana na sura yake kufanana na watu wenye asili ya Uchina.

Alipokuwa bado mdogo alikuwa akisakata kabumbu katika academy ya Danubio Fc, academy iliyowatoa pia Diego Forlan pamoja na Edinson Cavani. Alikuwa anauwasha moto balaa mpaka pale alipoonekana na mwamba wa kuitwa Sandro Mazolla, huyu Sandro alikuwa gwiji la Inter Millan kwenyw miaka ya 1960.

Baada ya kuvutiwa na uwezo wa dogo, akawasiliana na mshikaji wake Massimo Moratti, mkurugenzi wa klabu ya Inter Milan na kufanya mipango ya kumsajili.

Paundi millioni 14, naam hii ilikuwa ni pesa ya kwanza na ya mwisho aliyoitamka dogo alipoambiwa kuhusu kusajiliwa. Ikabidi Inter waitoe na kumchukua fundi huyo.

Akajiunga na Inter na mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Brescia ambapo alishinda goli zote mbili kwenye ushindi wa goli 2-1, ambapo goli la kwanza alipiga kombora kutoka umbali wa yard 40 na kufanikiwa kufunga, huku goli la pili akifunga kwa mkwaju wa Free kick. Kwenye mechi ambayo alimfunika partner wake kwenye ushambuliaji Ronaldo de Lima.

Lakini baada ya msimu mmoja akatolewa kwa mkopo kwenda Venezia ambako huko nako aliuwasha moto kwa kufunga goli 11 kwenyw michezo 19 aliyoichezea huku akiinusuru timu hiyo isishuke daraja. Wakati anaondoka kwenye timu hiyo wachezaji wenzake walimpa zawadi ya saa, sio kwa sababu ya magoli yake lah ni kwa sababu jamaa alikuwa ni bingwa sana wa kuchelewa mazoezini.

Kwa kiwango alichokionesha Inter Milan walimrudisha huku Massimo Moratti akimlipa kiasi cha paundi million 4 baada ya kodi na kumfanya kuwa ni mchezaji anayepokea mkwanja mrefu zaidi duniani kwa wakati huo.

Msimu wa 2002/2003 ulikuwa ni bora sana kwake pale Inter chini ya kocha Hector Cuper. Ambapo mwaka huo alisajiliwa Hernan Crespo ili kumrithi Ronaldo de Lima, na kuunda utatu mtakatifu ( Recoba, Vieri na Crespo). Jamaa alikuwa hapendi sana mazoezi lakini alikuwa anapata sapoti ya kutosha kutoka kwa Mkurugenzi wa Inter bwana Massimo Moratti aliyewekeza pesa zake za kutosha pale. Lakini kwenye mechi ya mwisho wa ligi dhidi ya Lazio Inter alipoteza goli 2-1 dhidi ya Lazio, ambapo kocha wa Inter akaamua kumtolea uvivu Recoba kwa kiwango kibovu alichokionesha siku hiyo.

Uongozi wa Inter ulibadilisha makocha kadhaa ili kumpata kocha atakayeendana na staili ya soka ya Recoba na wakampata Alberto Zaccheroni ambaye aliweza kumpa Recoba jukuma la kuwa "Free role player". Aliendelea kuuwasha moto lakini majeruhi yalimpenda zaidi kutokana na kupenda kwake starehe na kutolenda mazoezi.

Mwaka 2007 alitolewa kwa mkopo kwenda Torino ili kuangalia kiwango chake baada ya kupona majeraha yake, lakini huko nako akapata majeraha mengine yaliyopelekea kuanza kuyumba kwa career yake kwenye soka. Hatimaye akauzwa kwenye ligi ya Ugiriki na safari yake kwenye soka la ushindani ikawa imeishia hapo, na alistaafu mwaka 2015.

Amakumbukwa kwa magoli yake ya mashuti makali ya nje ya 18, na pasi zake murua kwa guu lake la kushoto.

Juan Veron aliwahi kunukuliwa akisema " Ukiniuliza kwa nini Recoba hakuwahi kuwa mchezaji bora, ni kwa sababu yeye mwenyewe hakutaka kuwa mchezaji bora"

Massimo Moratti na yeye alipoulizwa akajibu "Sijui, kwa sababu nilimpa kila kitu na kumpendelea zaidi kuliko Ronaldo".

Ulikuwa nami Aaron Arsenal
 
2002 aliuwasha motto wa hatari kombe la dunia dhidi ya Senegal.Senegal walitangulia 3-0 first half, second half Uruguay wakachomoa,Alvaro Recoba na Diego Forlan walikichafua ile charara. Kama ingeongezwa hata dakika tatu, Senegal wangekula hata Tano!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…