Unaniudhi wewe.....Wewe usiojua vema matumizi sahihi ya herufi...
Utakuta mtu hajui atumie wapi 'l' na wapi atumie 'r', anabaki kuchanganya na kuleta maneno au sentensi isiyoeleweka vizuri. Mfano, badala ya kuandika/kutamka 'Iringa' anatamka 'Ilinga'; badala ya 'Arusha' atasema 'Alusha'; badala ya 'rais' anatamka au ataandika 'lais'. Akitaka kusema 'ilani' yeye atasema 'irani'.
Kuna mwingine naye anaudhi sana tu, yeye hajui atumie wapi 'dhi' na wapi atumie 'zi'! Utakuta anataka usema 'maudhui' atakachosema ni 'mauzui' au anataka kusema 'maradhi' atasema 'marazi'.
Jirekebishe!