Unanunua MB utumie kote, SMS inakuja umenunua MBs za WhatsApp. Wanaomlinda mlaji wako wapi?

Unanunua MB utumie kote, SMS inakuja umenunua MBs za WhatsApp. Wanaomlinda mlaji wako wapi?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Salaam wana jukwaa,

Kumekuwa na tabia ambayo kwa sasa imekuwa sugu sana kwa hizi kampuni za mawasiliano kuamua kupanga bei za vifurushi na kuvibadilisha wanavyoona wao bila hata kuangalia mlaji au mteja wao wanampa usumbufu wa kiasi gani.

Kero hiyo haiishii tu kwenye kubadilisha bei za vifurushi bali hata unaweza nunua data mara unakutana na ujumbe hongera kwa kununua kifushi cha data za WatsApp au Youtube tu nk hali lengo lako lilikuwa ni upate data ambazo zitakuwa huru kutumika kwa matumizi yote ya kimtandao bila kubagua upande wowote.

Wakati mwingine unajiunga bandle linaisha ndani ya muda mfupi tena kwa matumizi yaleyale ya kila siku ambayo kimsingi huwa unatumia kwa muda mrefu, au unajiunga mtandao unakata huwezi tumia na muda ukifika wa kufikia mwisho wa matumizi linaisha bila kujali kuwa chanzo cha kutotumia ni wao kusumbua mtandao.

Nachojiuliza mamlaka ya kumlinda mlaji hawaoni jinsi mlaji wa hivi vifurushi vya data ambavyo anatendewa ndivyosivyo? wao wako wapi mbona hatuoni wakitututea ili tupate kile ambacho tunakusudia?
 
Hatuna pa kwenda kulalamika.

TCRA ukiwaambia wanaanza kudai ushahidi. Sijui wao huwa wanaregulate nini..

Yote tisa kumi yataisha endapo sisi wenyewe watanzania tutajitambua na kutaka maendeleo ya kweli
 
Back
Top Bottom