thegalaxy
New Member
- Jul 19, 2024
- 3
- 4
Mara zote ndoto huongea ukweli kwasababu ndoto,ni taarifa inayotokea katika ulimwengu usio na maamuzi ya kibinadamu...na ulimwengu huo huwa hausemi uwongo.
Ndoto huwa inaonekana ya uongo kwasababu, aliyeitafsiri ameitafsiri tofauti na ukweli ulivyo...hivyo huonekana kama ni haikua na maana.
Ndoto inayojishikiza katika fahamu zako,na ukaweza kuikumbuka hata ukiamka, si ndoto ya kuipuuza.Ndoto za namna hiyo hubeba taarifa muhimu ambayo kama utaijua inaweza kukuepusha,au kukamilisha jambo.
Uwezo pekee ambao Mungu kampa mwanadamu ni ule wa kuwasiliana na ulimwengu wa kiroho,ulimwengu wa jicho la tatu, ambalo jicho hilo lina uwezo wa kuiona kesho yako.
Fahamu hakuna kitu kinachokujua wewe zaidi ya nafsi yako mwenyewe, nafsi yako yajua ukweli wa maisha yako yote na fahamu kuwa nafsi ndio kiungo mkuu wa ulimwengu wa roho na ulimwengu wa kifizikia.
Ndoto ni uhusiano wa ulimwengu wa kiroho na ulimwengu wa kifizikia.Taarifa inayobebwa na ndoto huwa ni kweli tupu, haina ubinadamu ndani yake na kama umeota jambo na halikutokea au likatokea tofauti,si kwamba ndoto ile ni ya uwongo hapana wewe uliyetafsiri au aliyekutafsiria alitafsiri isivyo sahihi sababu taarifa ya ndoto hubeba ukweli pekee.
Na mara nyingi ndoto huhusiana zaidi na maisha yako binafsi ya kila siku,iwe familia,kazi,marafiki,ndugu n.k
Fahamu ukiwa hujalala usingizi una ufahamu wako, ni wakati ambao utashi hua na nguvu zaidi ya nafsi.
Binadamu unapo kuwa na fahamu utashi ndio hujaribu kukupa majibu ya maisha yako, hujaribu kuyachambua mambo katika hali ya ubinadamu na ulimwengu wa kifizikia,mfano kutatua changamoto mbalimbali zinazo kukabili.
Taarifa za maisha za binadamu yoyote hutunzwa katika ubongo.Na pale binadamu anapolala mwili wake pamoja na utashi wake huingia hatika hali ya kuto jitambua.Unapolala utashi na mwili hupoteza nguvu zake za kiutawala,na nafsi huchukua utawala huo.
Fahamu kuwa Nafsi yako haijawahi kulala,na haitakuja kulala,hata ukifa inaondoka haifi na wewe.
Hivyo unapolala usingizi mwili wako huingia katika hali ya kutojiyambua na ni wakati huo taarifa za maisha yako huwa wazi katika ulimwengu wa kiroho kwani nafsi yako ndio wakala au mesenja wa ulimwengu wa roho na ulimwengu wa kifizikia.
Na ufahamu kuwa nafsi yako,ndiyo msiri mkuu wa maisha yako,nafsi yako huwezi ificha chochote inajua siri zako,mabaya yako,uovu wako,na usafi wako,matatizo yako,na furaha yako.
Unapo lala nafsi yako hubeba taarifa zako zote,zikiwemo siri zako,ambazo labda hakuna binadamu kwenye ulimwengu wa fizikia anazijua,lakini nafsi huzijua na hubeba taarifa hizo zote hadi katika ulimwengu wa roho ili kupata majibu na maelezo katika ulimwengu wa roho kuhusu kesho yako.
Hivyo katika ulimwengu wa kiroho hakuna kisichojulikana kuhusu wewe.
(Kama utataka uufiche ulimwengu wa kiroho usijue chochote kuhusu mambo yako,basi izuie nafsi yako isijue siri zako na hiyo haiwezekani hadi siku unageuka kiwa maiti nafsi nayo ndiyo itakuachia hapo na kuondoka zake kurudi katika ulimwengu wa kiroho na mafaili yako.)
Baada ya ulimwengu wa roho kupitia taarifa za maisha yako,Nafsi yako tena huleta taarifa za kesho yako katika hali ya kuota.
Unapo ota hua ni kama uhalisia wa jambo lililotokea ambapo,taarifa za ulimwengu wa roho hujiandika katika ubongo wa kumbukumbu,ili mwanadamu huyu akiamka aweze kusoma taarifa hizo na aweze kuzitafsiri,ili kujiokoa,kutatua,kutimiza jambo flani linalokuja mbele yake.
Ndoto hua katika Lugha ya kiroho au inaweza kua katika lugha ya kisaikolojia,hivyo ndoto haina tafsiri sisi,ni lazima uwe mtaalamu wa kiroho au kisaikolojia kutafsiri ndoto kifasaa.
Japo kuna ndoto ambazo hua ni nyepesi kusitafsiri hata kwa mtu wa kawaida.
Hivyo kama kuna ujumbe wowote ambao nafsi imeubeba kutoka katika ulimwengu wa roho,fahamu kua ni lazima ujumbe huo utajiandika katika kumbukumbu ya ubongo wako na ukiamka utakumbuka kila kitu.
Kama hakuna ujumbe wowote muhimu ulioletwa,hautaota ndoto ambayo unakumbuka,utaota ndoto ambazo hutakumbuka.
Kama nilivyosema awali taarifa za ndoto mara nyingi hubeba ujumbe wa kesho yako.Na hivyo ndivyo mwanadamu anavyo wasiliana nguvu zilizo katika ulimwengu wa kiroho.
Ila tukumbuke kuwa kuna ulimwengu wa roho aina mbili.Ulimwengu wa roho zilizo Njema na ulimwengu wa roho zilizo Mbaya..
Nafsi yako inapoingia katika ulimwengu wa roho,hupita hatua na mbingu nyingi kabla ya kufikisha na kurudisha ujumbe.
Katika mchako huo taarifa za ndoto hubaki kuwa siri ya nafsi na huhakikisha taarifa zile zinafika bila kuvuja katika mbingu husika,ambako ndiko kuna roho wa Mungu mmiliki wa nafsi zote.
Lakini mara nyingine nafsi ambayo haijatakaswa na mwili,au tunaita nafsi iliyo chafuliwa na mwili hukosa nguvu ya kufika mbingu kuu ya roho wasafi na hujikuta ikivujisha siri za mwanadamu katika mbingu zenye roho wachafu..
Taarifa hizo zinapovuja, roho wachafu huweza kuzitumia taarifa hizo vibaya dhidi ya binadamu husika.Hapo ndipo wachawi na mapepo huweza kuchukua siri,na taarifa yako na kujua udhaifu wako na hata labda kukudhuru kirahisi.
Sababu ukumbuke pia nafsi nazo hukengeuka,kama tu mmiliki wa hiyo nafsi ni mchafu na ni mtu asiye itakasa.
Ila tukumbuke kuwa kuna binadamu ambao wamemkana Mungu(roho safi) na wamempokea Shetani(roho chafu) kwa hiari zao, hivyo si kila mtu hutegemea kupata ndoto kutoka roho wa Mungu,kuna watu ambao kupitia utashi wao na miili yao, wamekana ulimwengu wa roho watakatifu na kuzinajisi nafsi zao, watu hao ambao wao wamechagua kumtumikia shetani, hao nao huota ndoto ambazo maono na taarifa zake zinakua hazijatoka katika mbingu kuu bali mbingu ya roho wachafu na Shetani.
Hawa nao huwa na maono na taarifa za maisha yao ya kesho,lakini mara nyingi ndoto za mbingu ya roho wachafu helenga katika kutekeleza uovu,dhuruma,kupiga ramli,kupumbaza na si kufanya yalio matakatifu.
Hivyo hakuna ndoto ambayo unaikumbuka ikakosa maana,haijalishi umeota nini kama tu unakumbuka ndoto hiyo ina tafsiri yake na ina umuhimu wake.
Kama unaona ndoto na khutaki kujua maana yake hii ina maana unapuuza sauti ya nafsi yako na unasikiliza zaidi utashi na akili yako pekee.
Ndoto zina mchango mkubwa kwa maisha ya binadamu katika kumpa taarifa ya kesho yake au jambo fulani, kama onyo,tahadhari,ujumbe n.k
Ili kuepuka kuota ndoto ambazo unahisi zinatokana na roho wachafu.Jitahidi kufanya ibada muombe Mungu wako, autakase mwili wako na usiutie anisi mwili wako kwa zinaa na uchawi,nafsi yako nayo itabaki kua safi na haitaingiliwa na mashetani.
Lakini pia tufahamu kuwa matatizo ya kiakili,huweza kuchapisha taarifa zisizo sahihi katika ubongo wako,na hali ambayo inaweza kupelekea changamoto zaidi kwa mhusika,hata ndoto zako zinaweza zikawa na tafsiri ya kisaikolojia zaidi kuliko kiroho.
Thegalaxy
|
|
|
*Social counselor
*Religion and mind Psychologist
*Unconscious mind,Dream therapeutic and analytic