Unapenda game unaijua call of duty wewe?

Unapenda game unaijua call of duty wewe?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
Hii ni balaaaa [emoji91][emoji91][emoji91]

Call of duty modern warfare III Ni game mpya itakayoachiwa mwezi Septemba tarehe 10 mwaka huu, ni game inayojihusisha na upiganaji kwa mfumo wa mission za kivita. Game hii imetengenezwa na kampuni ya sledgehammer na kuachiwa na Activision.

Toka kuachiwa kwake mpaka Leo hii ni game ya Ishirini kwenye series zote za call of duty lakini ni Series ya Tatu kuachiwa toka kwenye series ya Modern warfare ambapo mwaka Jana 2022 iliachiwa Modern warfare II.

Game hii inahusu muendelezo wa afisa wa CIA Na kikosi Cha SAS toka uingereza wanashilikiana na waarifu (waasi) wa jamhuri ya kubuni ya Urzkistan. Wakipambana kwa pamoja dhidi ya wanajeshi wa kirusi.

Waliovamia nchi hiyo na kundi la kigaidi la Urzik Al Qatala wakati wakitafuta shehena ya gasi ya klorini iliyoibiwa kwenye meli na Ndege.kwaiyo kikosi Cha watu wanne kinatumwa kuokoa jahazi kiambatana na captain Price? Je wataweza? Tusibire Septemba 10 itakapoachiwa.

Game hii Ina muundo wa aina Mbili Kuna multiple player ambayo mnaweza cheza wawili lakini online pamoja na single player anacheza mmoja. Pia hii ndo series ya kwanza kwenye Call of duty modern warfare kuwa na mazombie yani Kuna missions mnacheza Kuna ma zombie sio poa.


Missions ziko zaidi ya 16 Kuna baadhi ya missions mpaka kumaliza inakuchukua masaa 10hr, nyingine, masaa 6hr, 12hr, 49hr masaa 9hrs na nk kwaiyo spidi Yako ndo kumaliza kwako[emoji87].

Ni game nzuri sana kuanzia mazingira unaweza sema kweli , Sauti inasikika balaa haswa ukicheza kwenye speaker za JBL , graphics yake ni nzuri ukianza kucheza hutaki kumaliza.

Game hii utaweza kucheza kwenye kompyuta, Ps 5 , PS4, Xbox Series ya X na S, Xbox One gharama yake ni Usd dollar 70[emoji383] weka oda Yako.

20230904_173829.jpg
 
Hii game huwa naielewa sana. Sema mission zake ngum kinoma mpaka utoboe inahitajika nguvu ya ziada.
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Ata kwenye PS3 unaweza cheza COD.

Nakumbuka nilikua nacheza COD Modern Warfare nikawa naweka Difficulty Advanced/Mature kama sijakosea. Wanakuambia kabisa You Won't Survive.

Aisee, ukibonyeza to Start haujui Sniper katokea wapi unakuta screen inajaa madamu damu.

Hii game COD na Assassin's Creed moja ya best games kwangu.
 
Nimecheza Game hizi za Call of Duty.
1. Call of Duty: World At War.
- Hii inatoa historia ya World War II, humo ndani ni balaa na nusu, vikosi vya Japan vinaua hatari.

2. Call of Duty Black Ops 1.
  • Hapa inaelezea vyombo vya ujasusi vya Russia vinamtengeneza kisayansi askari wa USA Alex Mason ili aje kuwa msaliti kwa nchi yake.
  • Lakini pia kuna black ops nyingi za maaskari wa US wanazifanya ktk mataifa mengine, mfano Cuba kumuua Fidel Castro. Black Ops ni operations za kijeshi za kisiri zinazoratibiwa na majeshi ya nchi kwa lengo maalumu hasa.

3. Call of Duty Modern Warfare 2 na 3, 4.
- Hizi ni kama zinatabiri kinachoendelea sasa duniani, jamaa wanaelezea Russia kuivamia Ukraine na vita vinapiganwa Ukraine, US anasaidia vikosi vya Ukraine kwa kutuma Makomando wake.


Hapa kuna missions nyingi sana, zingine zinaonesha vikosi vya Russia vimeteka na kufanya vita ktk ardhi ya US. Kuna balaa haswa ktk hizi Games. Ni vyema mtu akaamua kuzipakua hizi games na kuzicheza ili kuondoa stress na kurefresh mind.
 
Back
Top Bottom