Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Kwa mtu yeyote ambaye ameshawahi kusafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine bila shaka atakubali kuwa ni bora usahau kitu kingine chochote wakati unasafiri lakini sio paspoti yako.
Soma pia:
Ukweli ni kwamba Paspoti ni kama funguo inayokuwezesha kuingia kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.
Ukweli mwingine ni kuwa hadhi ya paspoti ya nchi moja hutofautiana na hadhi ya paspoti ya nchi nyingine.
Mathalani, hadhi na nguvu ya pasipoti kutoka Tanzania ina utofauti mkubwa sana na nchi nyingine kama Marekani, Nigeria au India. Hazifanani.
Na ndio maana taasisi tofauti tofauti ikiwemo Henley Passport Index na Nomad Passport Index kila mwaka hutoa orodha ya nchi zenye pasipoti zenye hadhi na nguvu zaidi duniani.
Sasa unaweza kuwa unajiuliza, ni vigezo gani wanatumia ili waweze kufahamu ni Pasipoti ya nchi gani ina nguvu zaidi. Baadhi ya vigezo ni
Maana yake ni kwamba Paspoti yenye nguvu zaidi ni ile inayokuwezesha kuingia kwenye nchi nyingi bila kuhitaji visa au makaratasi mengi.
Kwa mfano kama Paspoti ya Marekani inaniwezesha kuingia kwenye nchi 70 bila kuhitaji visa wakati Paspoti ya Kenya inaniwezesha kuingia kwenye nchi 90 maana yake ni kwamba, Pasipoti ya Kenya ina nguvu zaidi
Nchi ambazo zina amani na utulivu pamoja na mazingira rafiki ya kibiashara Paspoti zao huwa na nguvu na thamani kubwa na ndio maana nchi kama Switzerland au Denmark, Paspoti yao huwa na nguvu zaidi.
Nchi zinazoruhusu uraia pacha kama Uingereza na Marekani pasipoti zao huwa na nguvu zaidi kuliko nchi zisizoruhusu Uraia pacha kama Tanzania.
Kulingana na ripoti ya Henley Passport Index hizi ndio nchi za Kiafrika zenye Pasipoti zenye nguvu zaidi pamoja na idadi ya nchi ambazo unaweza kuingia kwa paspoti yao tu bila visa.
Nchi Zenye Pasipoti Zenye Nguvu Zaidi Duniani
1. Singapore - 195
2. France, Germany, Italy, Japan, Spain - 192
3. Austria, Denmark, Finland, Ireland, Luxembourg, Netherlands, South Korea, Sweden - 191
4. Belgium, New Zealand, Norway, Switzerland, United Kingdom - 190
5. Australia, Portugal - 189
6. Greece, Poland - 188
7. Canada, Czechia, Hungary, Malta - 187
8. United States - 186
9. Estonia, Lithuania, United Arab Emirates - 185
10. Iceland, Latvia, Slovakia, Slovenia - 184
Passport Zenye Nguvu Zaidi Barani Afrika

- Visa Free Travel

- Sera ya kodi
- Hadhi ya kimataifa
Nchi ambazo zina amani na utulivu pamoja na mazingira rafiki ya kibiashara Paspoti zao huwa na nguvu na thamani kubwa na ndio maana nchi kama Switzerland au Denmark, Paspoti yao huwa na nguvu zaidi.
- Uraia Pacha
Nchi zinazoruhusu uraia pacha kama Uingereza na Marekani pasipoti zao huwa na nguvu zaidi kuliko nchi zisizoruhusu Uraia pacha kama Tanzania.
Kulingana na ripoti ya Henley Passport Index hizi ndio nchi za Kiafrika zenye Pasipoti zenye nguvu zaidi pamoja na idadi ya nchi ambazo unaweza kuingia kwa paspoti yao tu bila visa.
Nchi Zenye Pasipoti Zenye Nguvu Zaidi Duniani
1. Singapore - 195
2. France, Germany, Italy, Japan, Spain - 192
3. Austria, Denmark, Finland, Ireland, Luxembourg, Netherlands, South Korea, Sweden - 191
4. Belgium, New Zealand, Norway, Switzerland, United Kingdom - 190
5. Australia, Portugal - 189
6. Greece, Poland - 188
7. Canada, Czechia, Hungary, Malta - 187
8. United States - 186
9. Estonia, Lithuania, United Arab Emirates - 185
10. Iceland, Latvia, Slovakia, Slovenia - 184
Passport Zenye Nguvu Zaidi Barani Afrika
- Seychelles - 156
- Mauritius - 150
- South Africa - 108
- Botswana - 91
- Namibia - 80
- Lesotho - 80
- Eswatini - 76
- Kenya - 76
- Malawi - 76
- Tanzania - 73