Kwa wale wanajamvi wanaopenda kusoma kwa upana (widely)kama mimi nina habari njema.
Leo hii katika pitapita yangu nimejikuta nikipita KASE Bookshop (Arusha) iliyopo jengo la KKKT ili kuona vitabu vipya vilivyoingia karibuni. huko nimekutana sale kabambe ambayo vitabu vya zamani vimetolewa nje na vinuzwa kwa punguzo la 30%.
Nimeishia kuzoa lundo la vitabu kwa sh 50,000 tu. baadhi ya vitabu hivi vilishapotea sokoni kwa hiyo hata bila punguzo ningependa nikinunue ili nipate kuongeza ufahamu wangu.
Hii ni fursa changamka.