Unapenda lipi? kutumia pesa yako au pesa ya wengine kufanya biashara

Sokoro waito

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
2,201
Reaction score
2,599
heshima kwenu wadau wa kutengeneza fursa za kuongeza utajiri,

wakati fulani niliwahi kusoma historia ya tajiri mkubwa aitwaye WARREN BUFFET, ambapo alielezea kwa ufanisi mkubwa kuhusu jinsi alivyoanza kuwekeza kwenye biashara huko marekani tangu miaka mingi iliyopita hadi leo hii amefikia hatua kubwa ya kumiliki utajiri mkubwa lakini kilichonishangaza zaidi ni pale aliposisitiza kuwa ni vizuri kuitumia pesa yako mwenyewe kwenye uwekezaji/biashara ama ujasiriamali kuliko kutumia pesa ya watu wengine kwenye biashara/uwekezaji ama ujasiriamali.

Tafsiri isiyo rasmi ya maneno, 'pesa yako' na 'pesa ya wengine' ni hii hapa chini;

'pesa yako' inamaanisha pesa unayomiliki wewe mwenyewe isiyomilikiwa na mtu yeyote yule isipokuwa wewe tu.

'pesa ya wengine' inamaanisha pesa inayomilikiwa na watu wengine ila waweza pewa kwa masharti maalumu kuitumia pesa hiyo, kwa mfano mikopo kutoka benki, mikopo kutoka kwa watu binafsi, nakadhalika.

tuambizane wakuu, je wewe unapenda kutumia pesa ipi kukuza biashara zako katika zama hizi? na kwanini?

je pesa ipi kati ya hizo inawasaidia wafanyabiashara walio wengi kufika mbali kibiashara?

karibuni kwa mjadala.
 
Pesa yako na pesa ya mwengine (combination) ukizitumia kwa nidhamu ya hali juu kwa kuzi heshimu utafika mbali
 
Pesa yako na pesa ya mwengine (combination) ukizitumia kwa nidhamu ya hali juu kwa kuzi heshimu utafika mbali
asante kwa mchango wako, kuelimishana ni jambo jema,

mbinu gani unatumia wakati wa kutumia pesa ya watu wengine ili ikunufaishe na kumnufaisha mwenye nayo pasipo kukuachia majuto baadae?
 
Mimi nitofautiane na wengine,kwangu napenda kutumia pesa ya mkopo kwenye biashara.Yani nikikaa bila biashara kudaiwa huwa sijisikii amani,mkopo uwa unanifanya niwe serious sana kwenye biashara.
Nilianza kwa mkopo na sitokuja kuacha kukopa,coz huwa nafanya ela ya mkopo kama business guider
 
siku ya kwanza kujarb kukopa nilienda kwenye saccos flan hv yan wakat nataka kutia sain natoka jasho mwili mzima , huwez amin mbele ya wakopeshaji nilighairi fasta, walishangaa sana mana nilitimiza vigezo vyote vya kupewa ambapo weng waliohtaj walishndwa. Natoka naenda nyumbn nilikutana na wezi hawakusubr nivue beg walilikata mikata wakalala mbele, kwa ufupi waliambulia kitab flan hv na bis za jero, nami nilitoka nduki nikajua wanaweza wanirudie. Niliwaza sana km ile hela yote ningeirudsha vp, tangu pale sipend kukopa japo siwez sema sitokopa, nafika nyumb kumbe na bimkubwa nae hakua na aman nilimkuta kashka shavu ananisubiria,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…