Unapigwa ulie halafu unapigwa Tena ili unyamaze.

Unapigwa ulie halafu unapigwa Tena ili unyamaze.

Raymanu KE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
8,611
Reaction score
16,118
Nakumbuka kipindi nikiwa mdogo nilikuwa msumbufu Sana na mama yangu alikuwa mnoko Tena mkali ajabu.Kipindi hicho wiki isingeweza kuisha kabla sijachezea mabakora ya mama kutokana na ununda wangu.

Nakumbuka visasa kadha wa kadha ambavyo vilinisababishia adhabu Kali Sana kutoka kwa mama.Kuna siku nilijumuika na rafiki zangu kuwapeleka ng'ombe machungani.Tulikuwa takribani watoto Saba tukawakusanya ng'ombe wetu kwenye uwanja mmoja huku tunacheza mpira mixer kuwapiganisha ng'ombe ndume.Ng'ombe wangu mmoja aligongwa vibaya Sana kwa kudungwa dungwa mapembe na ng'ombe mwingine Hadi akafumuliwa kipande Cha ngozi.

Nilirudi nyumbani natetemeka Sana maana nilijua naenda kuchezea kichapo sio Cha sayari hii wakuu.Nyumbani palichimbika kinyama Yaani nilipigwa mafimbo mengi Sana nikalia Hadi nikazimia.Yaani unapigwa unalia Kisha unapigwa Tena ili unyamaze [emoji23].Ukishapigwa unaambiwa uchukue maji ya baridi uoge Kisha uende chumbani ukalale, chakula unanyimwa[emoji25]

Kisa Cha pili ile umerudi shuleni jioni kabsa kisha mama anakuamuru uchukue mtungi uwahi mtoni ukateke maji ya kunywa.Jamaa nazuga kuwa nimeenda mtoni kumbe nimepitia kwa rafiki yangu kucheza kibe.Giza kinaingia mtoni sijaenda na nyumbani wamesubiri maji.Nikaamua kuchota maji ya kisima na kurudi nyumbani.Kwa ujinga wangu kamwe sikuwahi jua kwamba ladha ya maji ya kisima Ni tofauti Sana na ladha ya maji ya mtoni.Mama akayaonja maji akakuta Ni ya kisimani kudadeki!!
Nilipigwa, nikachunwa,nikatukanwa mixer kunyimwa chakula.Usiku wa manane njaa imekuchachamaa unaanza kulia mama anaamka anawasha taa anakuja ananichapa Tena ili ninyamaze kulia.

Kipindi Cha utoto wangu nilipitia Mikasa mingi Sana ambayo siwezi kuielezea yote lakini ilinisababishia adhabu Kali Sana kutoka kwa mama.Lakini namshukuru Sana mama yangu coz adhabu zake zilininyoosha na kunifanya niwe na nidhamu ya Hali ya juu.Mungu ambariki mama yangu[emoji120][emoji120]
 
Mama yako mkatili abadani asilan siwezi mnyima mtoto wangu chakula au watoto
Nikimchapa huwa naumia mno nishaacha kabisa nimebakiza mdomo kuongea tu
 
Hizi adhabu za ajabuajabu ndiyo zinatuzalishia viongozi na polisi watiifu tulio nao leo.
 
Matendo Kama hayo yame changiwa mnoo kuzalisha chuki kwa watoto dhidi ya wazazi wao bila wazazi wao kujua kuwa wanapandikiza mbegu ya chuki katika vifua na fikira za watoto wao , Na ndio maana jamii yetu umekuwa na watu wengi wanao Amini katika ugomvi na mapigano kuwa ndio njia sahihi ya kutatua matatizo wanayo kutana nayo,, Pia tusishangae Sana kuona baadhi ya watoto wakiwaua wazazi wao yote Ni kwa sababu miongoni mwa hao wauaji wapo watu waliopitia katika makuzi ya Aina hiyo na hatimae wakijikuta Wana kuwa watu wazima huku wakiwa wame athirika kisaikolojia dhidi ya wazazi wao , na kuwaona kuwa Ni watesi wao , people's we need to change ,

Ni ukweli uliowazi kwamba wazazi wengi wa kiafrica waliathiriwa kitabia na mfumo wa kikoloni uliokuwa una Tawala nyakati hizo zilizopita , kwa kuwa ulikuwa Ni mfumo onezi na wenye ukandamizaji na wao wakajikuta Wana upokea na kuufanya kuwa ndio falasafa ya maisha yao ,(Yaani ubabe ubabe tu , [emoji16][emoji16] ,) ule Ni ujinga Yale sio malezi Mtatuzi wa malezi Bora Ni akili na sio matumizi makubwa ya nguvu kwa kizazi chako
 
Back
Top Bottom