Unapofanya jambo lako kumbuka pia kuna kufeli na changamoto zake

Unapofanya jambo lako kumbuka pia kuna kufeli na changamoto zake

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
Biashara, mahusiano, mipango mingi inafeli sababu watu hawajiandai na changamoto za anachokitafuta ama kukifanya matokeo yake anawaza faida tu, zinapokuja changamoto zake anajikuta anafeli kirahisi sana.

Biashara nyingi zinapoandaliwa huwa ni kwa mpango wa "high season" mauzo yako juu lakini uhalisia hakuna biashara ambayo inakuwa kwenye high season mwaka mzima ni lazima kuwe na kipindi cha "low season" mauzo hafifu na hapo ndio biashara nyingi hufa, kwa kuwa hazikujiandaa na low season matokeo yake ni kula mtaji na kupumzika, hili ni janga la biashara nyingi.

UNAPOTENGENEZA MPANGO WAKO WAZA NA KIPINDI CHA KUFELI AMA KUPOROMOKA KWA BIASHARA UTAFANYA NINI

Kwenye mahusiano wapenzi wengi huingia wakitegemea raha tu na furaha na mara nyingi mwanzo wa mahusiano kila mtu hujitahidi kufanya ili kumridhisha mwenzake,ila baada ya muda ile hali ya kuridhishana huisha huingia hali ya uhalisia hapo ndio shida huanza, vikwazo, wivu,husda, vijitabia huonekana, sasa kwa kuwa akili ya wengi huwa ni mpenzi wako ni furaha yako 100% hujikuta wanaumia sana na kufeli kuendelea ama hata kutengeneza magonjwa ya hisia.

ILI UDUMU NA UISHI VIZURI KWENYE MAHUSIANO ONDOA HALI YA UMILIKI NA WEKA HALI YA URAFIKI, MCHUKULIE MPENZI WAKO KAMA RAFIKI YAKO, HATA AKIKUUDHI UTAWEZA MSAMEHE NA KUENDELEA KAMA UNAVYOFANYA KWA RAFIKI YAKO.

Mipango mingi inafeli sababu watu hawafikirii upande wa pili wa mpango iwapo utafeli itakuwaje, pale inapotokea imeenda kinyume na matarajio watu hughafirika na wengine hutengeneza magonjwa (Mshtuko wa moyo, presha n.k)

UNAPOTENGENEZA MPANGO WAKO WOWOTE WEKA NA ASILIMIA ZA KUFELI NA IWAPO UKIFELI WEWE UTAFANYA NINI AMA KUWA KWENYE HALI GANI?

Maisha ni haya haya, wakubadilika ni wewe, wazazi wafundisheni watoto maisha sio kushinda tu kuna kufeli ambako ni sehemu kubwa ya kujifunza, ili waweze kukabiliana na hali za kufeli, kukataliwa, kudharauliwa, kubezwa katika maisha yao.

Elisha Chuma
Mwalimu & Mshauri Maisha, Ujasiriamali Biashara na Uchumi


IMG_20200406_093758_146.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha ni haya haya, wakubadilika ni wewe, wazazi wafundisheni watoto maisha sio kushinda tu kuna kufeli ambako ni sehemu kubwa ya kujifunza,ili waweze kukabiliana na hali za kufeli,kukataliwa, kudharauliwa,kubezwa katika maisha yao.

Umenena vyema sana, ila nadhani hii inapendeza vizuri zaidi kama unakua umeandika kabisa. Hizi expectations za kwamba nitafanikiwa tu kama watu wa Qnet au Alliance Global in Motion na nduguze ndio mbaya zaidi.

1586156153785.png
 
Back
Top Bottom