Unapoibiwa benki

Unapoibiwa benki

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
8,191
Reaction score
8,490
NAomba kuuliza,sheria inasemaje kuhusu haki ya mtu aliyeibiwa ndani ya benki wakati wa tukio la ujambazi kabla hajakabidhi fedha hizo kwa muhusika wa benki.
 
Mkuu sheria hii sijui inasemaje lakini nahisi benki haihusiki na wizi huo. Pia hakuna udhibitisho kuwa ulikuwa na fungu mkononi.
Sijui lakini, wanazuoni watusaidie katika hili.
 
Mkuu sheria hii sijui inasemaje lakini nahisi benki haihusiki na wizi huo. Pia hakuna udhibitisho kuwa ulikuwa na fungu mkononi.
Sijui lakini, wanazuoni watusaidie katika hili.

Labda kama anaweza kuthibitisha kuwa benki ilishirikiana na majambazi hayo. Otherwise sioni chance ya muathirika kufungua any 'winnable' case against the bank.
 
Very much so, ulinyoenda kuweka hela benki ulikuwa umeenda pale kwa mwaliko wa benki. Kwa mwaliko huo benki ilitakiwa kuona na kuchukua tahadhari kuwa hakuna madhara yoyote yanawafikia waalikwa wao katika premises zao.

Kama kweli ulikuwepo nenda mahakamani, spidi 180 kwa saa.
 
Kama bado haujaweka bank hiyo bado ni mali yako na unatakiwa kuilinda kama vile ukiwa umevaa saa yako ya thamani na kupita sehemu ambazo ni makazi ya vibaka.
Kwahiyo basi ukiibiwa hela ndani ya bank ni sawa tu na kama vile ungeibiwa ukiwa Tandale au Uhafiwa!
 
Ukiwa Tandale au Uhafiwa usalama wako uko juu yako, umekwenda pale kwa hiari yako, lakini ukiwa benki kwa minajili ya kudeposit hela basi umekaribishwa na benki na kama benki imekukaribisha basi wanawajibika kwa kila hali na usalama wako na mali zako.

Haitajalisha kama umedeposit fedha hizo benki au la.
 
Back
Top Bottom