Unapojihisi mpweke...

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Unapohisi kum miss mtu aliye mbali nawe, ukumbuke mwezi.
Licha ya kuwa umbali wa maelfu ya maili, Lakini uko karibu zaidi kuliko vile unavyofikiria, maana unautazama mwezi huo mmoja Kula usiku.

Unapohisi kupotea na kutokuwa na uhakika na kuchanganyikiwa, fikiria kuhusu mwezi. Ni mwezi uleule uliokuwa ukiutazama kwa macho ya matumaini ulipokuwa mtoto mdogo. Haujawahi kubadilika.

Unapopata hofu na siku zijazo na wakati unakimbia, fikiria kuhusu mwezi. Ukiwa na umri wa miaka 80, utautazama mwezi uleule utakaouona usiku wa leo, kwa macho ya machozi, na kujivunia utasonga mbele na kushukuru sana kwa maisha ambayo umeishi.πŸ’ͺπŸΏπŸ‘ŒπŸΏ

Na unapofikiri huna chochote kilichobaki, bado kumbuka una mwezi wa kuutazama usiku wa leo.. Utakaokumulikia na kukuongoza kwenye kiza tororo cha kukata tamaa, wasiwsi na mapito ya maisha
 
Hujawahi kuumizwa na mapenzi wewe.
Sema sahv nimekomaa, nitakuwa nauangalia mwezi Mshana Jr
 
Ebhan!!!,duh mkuu huu Uzi umetulia japo bado nashindwa kuuelew.naomb unidadavulie mkuu
 
uzi mzuri Sana, wa kuongeza matumaini pale ambapo tunahisi kupungukiwa mahali na kuihataji matumaini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…