MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,580
Maisha ya ndoa na mahusiano ni kama kuna maboksi ambayo tunatamani kuwa nayo na kuyabeba maisha yetu yote. Wengi wetu hupata bahati ya kupata mabox mema na wengine huambulia mengine ambayo tungejua tungefikiria kwanza kabla ya kuamua kuyabeba!
Wengi wetu tumejikuta tumebeba maboksi ambayo tunadhani ni yetu na kwa furaha kubwa huwa tunawaringishia wengine hasa kutokana uzuri wa boksi kwa nje tukitegemea na ndani litakuwa na kitu kizuri.
Hata hivyo tukifika majumbani tunashangaa huku vitu vilivyomo ndani ya boksi ni kinyume chake. Mara nyingi tunaambulia maboksi ambayo ndani yake yamejaa viboksi vingine vingi kama vile hasira, ukali, au manyanyaso ya kila aina, maneno magumu na mazito ambayo hukuumiza zaidi ya kupigwa ngumi na mateke.
Mbaya zaidi pale pale box lenyewe likijua kwamba wewe ni mbebaji mzuri basi utachakaa kwa kubeba hili boksi.
Hali hii huitwa Narcissism hili ni neno la kigiriki lenye maana ya mtu kuipenda zaidi nafsi yake kuliko kawaida (extreme self-loving). Tatizo ambalo huanzia utotoni baada ya mtu kukosa upendo so anapokuwa mtu mzima anakuwa hajui maana ya kupenda na kupendwa.
Utafiti unaonesha ni asilimia 75 wana kaasili ka narcissists na kinara wao akiwa Adolph Hitler. Wengi wetu tunao akina Hitler kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi. Pale ambapo mpenzi wako anachofanya ni kukubebesha kiboksi cha wewe Kujiona una hatia, anakupa hofu, woga, mashaka, anakufanya usijiamini ili akupelekesha anavyotaka yeye. Wakati mwingine anaweza kudhalilisha kimwili, kimapenzi, kihisia na pia anaweza kuzira kuongea (silence) na anachofanya ni kuku-control wewe idara zote za maisha yako unakuwa kama mfungwa fulani kwa kuwa umeingia kwenye anga zake.
Wapenzi wa namna hii wanaume au wanawake hufurahia sana kutesa wake zao au waume zao, hawana huruma wala haya.
Source:The Hill Of Wealth
Je unapojikuta unaye mtu wa hivi na wewe umeolewa/ oa kanisani ndoa ya kikristo. Unafanyaje?