Unapokuwa na Mpenzi wako mpya!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,794
Reaction score
9,075
Hivi wakuu unapopata mpenzi wako mpya na mapenzi ndo kwanza ya motomoto ikatokea akapigiwa simu na na XBoyfriend wake kwanini wanaume huwatuna chukia nakunung'unika mpaka kumwambia mpenzi wako mimi sitaki uendelee kuwasiliana naye??lakini wewe ukipigiwa poa tu na unamwambia huyo ni Xgal wangu namwambia kwamba kwasasa aachane na mimi nimeshampata nimpendaye na Huyo mpenzi wako halalamiki!!Hila wewe akipigiwa simu yeye unakasirika wakati unajua fika huko nyuma alikuwa na mtu napengine wewe ndiye umevuruga uhusiano wao!!Nikwanini??Tujiulize!
 


Ubinadamu kazi kwelikweli, na hasa unapokuwa mwanaume!
 
Sense of Insecurity kwa kidume... dume linahisi demu atarejsha majeshi... kumbuka wanawake ni wepesi kurudisha roho nyuma na wanaweza kupenda tena huko walikotendwa!! kwa kuchimba biti jamaa anajaribu kulinda windo lake bana!:eyeroll2:
 
Mara nyingi unakosa amani hata unapopishana na ex wa mkeo, unless unafahamu fika waliachana vipi. Ukifiria kuwa msema kwaheri kwa wema, basi abishapo hodi hukaribishwa tena...! Hivyo, ukiona kama bado kuna mawasiliano, basi kuna kila ishara ya kurudiana. Lingine ni kwamba, lazima yule ex wa mkeo atakuwa amemfahamu mkeo vizuri sana, (areas of weaknesses and strengths), hivyo kama umakini hautatumika, mara nyingi sisi wanaume tunaweza kutumia hizi opportunities kukumbushia ya zamani....! Hata hivyo wanawake huwa wakisamehe wanajua kusamehe, misamaha hutolewa bila mipaka...! Na ukumbuke kuwa ukimsamehe ex wako kwa kosa lililowatenganisha, basi kuna uwezekano mkubwa sana kurudiana...! Hata kama umesababisha wewe kuachana wao, uonapo mawasiliano kama haya utafikiri kuwa wewe bado hujaweza kumridhisha mkeo kiasi cha kuachana na yule ex wake.

ONYO:

  1. Mawasiliano kwa ex wako ni sumu kali sana kwa mahusiano yako ya sasa.
  2. Wahenga husema, "Usinyee kambi", lakini kambi ya mapenzi inapovunjwa ni muhimu kuinyea kabisa.
  3. Kamwe usikubali kuishi na mtu aliyeagana na ex wake kwa amani...! You will be into a very big risk.
 

Duh! :confused2:
 
unajua kuna karha sana kwa mwanamke kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja lakini hiyo sio sawa na kwa mwanaume
 

Halafu KakaKiiza hii topic yako imenikumbusha 80/20 rule
 
Wanaume tuna wivu sana kuliko wanawake
 
Kweli TUPU.. Ni wivu tu UNASUMBUA... Tunawaonea sana hawa watu!
 
inategemea wameachana kivipi kama hakukuwa na mgogoro mkubwa wanaweza kurudiana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…