Unapokwenda kuomba mkopo bank unakumbuka kusoma vigezo na masharti?

Unapokwenda kuomba mkopo bank unakumbuka kusoma vigezo na masharti?

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Poleni sana ndugu zangu, naona maisha yamewapiga sana mpaka nafikiria kufungua miradi mingine niwaajiri wote.

Tuachane na hayo, leo nilikuwa kwenye bank moja nikashuhudia kitu cha kushtua kidogo, jamaa alikuwa anajaza form ya mkopo, yaani hasomi terms and conditions yeye anaoneshwa saini hapa anasaini, na hapa anasaini, na hapa anasaini.

Hii imenitisha sana, kwanini unapohitaji mkopo usijipe muda wa kusoma vigezo na masharti ukishindwa kuelewa tafuta laki 2 mwombe mwanasheria akueleweshe vipengele vyenye utata ili usaini kitu unacho kielewa.

Huyu mwamba kasaini kama radi kisha akauliza ni lini pesa inaingia akaambiwa mpaka mwajiri wako a approve ila ni ndani ya siku 2. Jamaa akasepa, sura yake inaonesha ni mtu mwenye shida kubwa ila shida isikuondoe akili.

Nikajiuliza kama viongozi hutokea miongoni mwa jamii na ikiwa jamii haina tabia ya kusoma terms and conditions kwanini nisishawishike kuwa viongozi wenu pia wanaweza kuwa hivyo? Yaani wanaweza kusaini mkataba bila kuusoma.

Asante.
 
Haujabanwa nashida ww...hizo akili hukurudia ukishakua umepata pesa mkuu.
 
Back
Top Bottom