unaponunua umeme unaingiza vitu viwili, mita namba na pesa
zinatumwa kwenye server, pesa inabadilika kuwa units (kulingana na tariff uliyopo), then units zinaungwa na mita namba pamoja, zao linakua encrypted then linakua encoded, kwa standards za STS (algorithm) , token inatoka na kutumiwa wewe
ukiingiza token kwenye mita, mita ina micro processor inafanya reverse ya kile kilichofanyika hapo juu kwa standard ile ile ya STS
token inakua decoded,decrypted , inapatikana mita namba na units
processor inaangalia mita namba ikiyopatikana inalandana na mita namba yako ? kama ndiyo units zinaingizwa na kuongeza umeme ,