Safety last
JF-Expert Member
- Mar 24, 2011
- 4,236
- 1,411
Kichaa siyo maradhi ,bali wataalam wengi wa saikolojia wanasema ni mtindo wa maisha ambao mtu ameamua kuishi.Nataka nikuulize swali hivi unapokwenda kuoa au kuolewa,ni nani atakwambia kwamba unayetaka kuoana naye ni kichaa?Hakuna.Unakutana mtu amevaa vizuri,amependeza,anafanya kazi yake na anaongea vizuri,unaamini kwamba ni mzima wakati mwingine amesoma sana pia "Hizo ndizo sababu zinakufanya usiulize hadhi yake kiakili"kuwa kichaa ni kuyatazama mambo kinyumenyume au kuyaona yale ambayo wengine hawayaoni katika hali halisi,huku ukijiumiza na kuwaumiza wengine pia.Kuna vichaa aina nyingi mfano:kupenda sana ngono ni kichaa,kupenda sana fedha ni kichaa, kupenda sana sifa na kujionesha ni kichaa,kupenda sana pombe ni kichaa, kupenda sana kukosoa na kulalamika ni kichaa,kupenda sana KUPENDWA ni kichaa na vingine vingi .Naita hivi ni kichaa sababu huo wote ni ukengeuko na unahitaji kupatiwa tiba hasa ushauri.Hebu fikiria umeolewa au kuoa kichaa mmoja kati ya hao hapo juu, Utafanyaje??