Unapooana na kichaa halisi !

Safety last

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
4,236
Reaction score
1,411
Kichaa siyo maradhi ,bali wataalam wengi wa saikolojia wanasema ni mtindo wa maisha ambao mtu ameamua kuishi.Nataka nikuulize swali hivi unapokwenda kuoa au kuolewa,ni nani atakwambia kwamba unayetaka kuoana naye ni kichaa?Hakuna.Unakutana mtu amevaa vizuri,amependeza,anafanya kazi yake na anaongea vizuri,unaamini kwamba ni mzima wakati mwingine amesoma sana pia "Hizo ndizo sababu zinakufanya usiulize hadhi yake kiakili"kuwa kichaa ni kuyatazama mambo kinyumenyume au kuyaona yale ambayo wengine hawayaoni katika hali halisi,huku ukijiumiza na kuwaumiza wengine pia.Kuna vichaa aina nyingi mfano:kupenda sana ngono ni kichaa,kupenda sana fedha ni kichaa, kupenda sana sifa na kujionesha ni kichaa,kupenda sana pombe ni kichaa, kupenda sana kukosoa na kulalamika ni kichaa,kupenda sana KUPENDWA ni kichaa na vingine vingi .Naita hivi ni kichaa sababu huo wote ni ukengeuko na unahitaji kupatiwa tiba hasa ushauri.Hebu fikiria umeolewa au kuoa kichaa mmoja kati ya hao hapo juu, Utafanyaje??
 
Reactions: Mbu
Ndo kazi ya urafiki, then uchumba ili upate kumchunguza na kumjua upendaye kwa undani zaidi.
 
Kama mtu anapima kila unachofanya mfano,anamwambia mwenzie juzi na jana nimekuoshea gari lako hata asante hunipi .huyo si mzima
 
Ndo kazi ya urafiki, then uchumba ili upate kumchunguza na kumjua upendaye kwa undani zaidi.

nazungumzia ulikuwa "HUJUI NA UKO KWENYE NDOA" kwamba mwenzako alishawahi kufanya vitendo vinavyoonyesha kuchanganyikiwa kama kutaka kuua mtu,kutaka kujiua mwenyewe,uadui na kila mtu,kuwanyang'anya wengine wapenzi,wake au waume,na mengine ya aina hiyo utafanyaje?
 
So that is your definition of "ukichaa"?
 
basi kila mtu anaukichaa wake! all mention above ni sifa za watu tofauti,issue ni kujuana ukichaa wa kila mmoja wenu then maisha yasonge mbele mkuu!
 
Ni afadhali kichaa anayevua nguo au kuropoka hovyo,maana huyu amepoteza uhalisi akiwa hajui,hawa vichaa ninaowasema ni vichaa wanaojua ni vichaa,lakini ni waoga wa kutaka kutoka kwenye vichaa.
 

kwa lugha ya kiroho huu ulafi tunautambua kuw ani laana ya ulafi......................au kwa lugha ya wenzetu ni......................a curse of consumption..........
 

Hapa wewe unaonesha dalili zote za ukichaa.
 

Kama ndo hivyo utakuwa hukufanya wide research kabla hujaoa/hujaolewa kwa kifupi ulikurupuka
 
Kama ni hivyo kila mtu ana kichaa na kama ukitaka kuolewa/kuoa kwakutaka ambae siyo kichaa unaeza usipate mwenza sema utafute ambae ukichaa wake unanafuu
 
Kwa tafsiri hiyo basi kila UDHAIFU wa mwanadamu ni U KICHAA.Kwakuwa binadamu wote si watimilifu kwa maana ya udhaifu,basi kwa mtizamo wako tu conclude kwamba watu wote ni vichaa,na hivyo hata ufanye utafiti wa kumpata asiye na kichaa kwa karne nzima huwezi kumpata!Kwa mantiki hiyo basi ni bora kuomba mungu umpate mwenza ambaye anakichaa POSITIVE.Kwa mfano yule anaependa sana KUPENDWA nk.
 
Kwa mimi ninavyoafahamu, kila mtu ni kichaa, isipokuwa degree ya ukichaa ndiyo imetofautiana! wengine wamezidi, wangine wamepungua. Ukitaka kuprove, mchokeza mtu yeyote yule utaona varangati litakalokupata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…