Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za wakati huu ma GTs
Poleni kwa changamoto ya Korona na ni matumaini yangu kwamba kila mmoja wengi tunapambana ili kuweza kuishi.Kama uliweka malengo mengi katika mwaka huu wa 2020 basi ni muhimu ukarekebisha malengo yako na kuweka lengo kipaumbele lako kuwa ni kuendelea kuwa hai."STAY ALIVE"
Jilinde wewe na wale uwapendao hakikisha unazuia maambukizi zaidi ya COVID 19.Ukiweza kubaki hai mpaka mwisho wa janga hili utakuwa umetengeneza faida maradufu.
Pamoja na hatua za kuchukua ili kujilinda ni muhimu pia ukachukua hatua za kulinda biashara yako. Hizi ni baadhi ya hatua za kuchukua ili kulinda biashara yajo katika kipindi hiki cha COVID 19:
STAY ALIVE, BE SAFE, PROTECT

- Kuwa muwazi na toa taarifa sahihi kwa wadau wako wakiwamo wateja,wafanyakazi,creditors,supplier etc.Usisingizie kila kitu kuwa ni CORONA.
- Punguza gharama za uendeshaji kwa kuepuka matumizi yasiyokuwa na lazima
- Thamini sana wateja wako wanaoendelea kukuunga mkono katika kipindi hiki kigumu
- Thamini sana wafanyakazi wako wanaoendelea kufanya kazi zako katika kipindi hiki cha COVID
- Iwapo inakubidi kufanya maamuzi magumu katika kipindi hiki basi washirikishe wote watakoathirika na wape nafasi ya kutoa maoni na njia mbadala
- Kwa wale ambao waliokuwa hawajatumia teknolojia wezeshi katika biashara zao ni muhimu sasa wakafikiri namna ya kuweza kuweka teknolojia ili kuwezesha shughuli za kibiashara kuendelea hata katika majanga kama haya.Teknolojia wezeshi ziko za aina nyingi ikiwamo mifumo ya mawasiliano, mifumo ya uhifadhi taarifa, Coworking, remote working, multi tasking n.k.
- Kwa wale ambao wana upungufu wa ujuzi ni wakati sasa wa kuchukua hatua ni kujifunza mambo mapya kwa kutumia teknolojia-Elearning
STAY ALIVE, BE SAFE, PROTECT