Unapotetea dhuluma maana yake umedhulumu taifa na vizazi vyote

Rule L

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2020
Posts
2,180
Reaction score
3,477
Kama kichwa cha habari kinavyosema ni kwamba unapotetea dhuluma ya aina yeyote ile basi umewakatili mamilioni ya watu kwa zaidi ya karne kadhaa.

Unapokua katika jeshi lolote lile na ukatetea dhuluma ama kusaidia kupora haki za watu basi utakua umejidhulumu hadi wewe mwenyewe.

Mfano, Askari police unapozuia watu kuomba haki yao maana yake umeshiriki kujidhulumu wewe mwenyewe, leo hii watu wanapolia mishahara ni midogo maana yake wamekutetea nawewe.
Sasa unapokataza hilo kwaposho ya elfu hamsini ama laki moja kwasiku maana yake wewe ni juha.

Haiwezekani laki ya siku moja ikuzuie kuomba kupandishiwa mshahara kwa miaka kadhaa utakayokuwepo kazini, hiki ni kiwango cha juu sana cha ujinga.

Vilevile una kaka,dada mama baba na watoto wako ambao utakua umewanyima haki ya kupewa maisha bora.
Inamaana gani kua sehemu ambayo unadhulumu ndugu zako wadamu??

Kumbuka maombi ya ndugu zako kijijiini kabla hujawa hapo ambao walidhani utawatetea baada ya kupata kazi.

Una ndugu masikini ambao hata kibiriti hawawezi kununua bali wanakonda na kubeba magogo ya kukoka moto wa moja kwa moja. Una ndugu ambao hata chai hawawezi kuipika maana hawajui hata viungo vyake ni vipi? Acheni mihemko. Siku wakija kwako hawataki kutoka maana wanajua wanarudi kwenye viporo vya ugali.

Lakini pia machawa kama akina lukas waliokosa akili kabisa unamtetea mtu ambaye hakanyagi chini anawekewa carpet ndio apite?? Je una kumbuka kwamba bibi yako kapelekewa kitambaa cha kichwani tu? Je wewe unayeishia kuvaa kepu??? Umewawazia watoto ambao wanasoma nje ya darasa???

Vipi kuhusu afya mbovu??? Una ndugu wangapi waliofariki kwa kukosa huduma bora?? Tuchukue hatua kila mtu kwa nafasi yake.

Ni muda sahihi wa kufanya maamuzi bora na kuviachia vizazi vyetu historia ya kipekee na ya kukumbukwa!

Ni muda wa kuidai haki kwa njia zote mpaka ipatikane.

FANYA MAAMUZI LEO UOKOE VIZAZI VIJAVYO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…