Unapoweka malengo ya kufanikiwa, zingatia jambo hili

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
1,684
Reaction score
2,156
Lengo Moja Muhimu Unalopaswa Kujiwekea 2020 Ili Uweze Kufikia Malengo Mengine Unayojiwekea.

Heri ya mwaka mpya 2020!

Ni nafasi ya kipekee sana kwetu tumeipata kuiona siku hii nyingine mpya, ya mwaka mwingine mpya. Siyo kwa nguvu zetu, wala kwa akili zetu, bali ni kwa neema tu. Hivyo tunapaswa kutumia nafasi hii vizuri, ili iwe na maana kwetu na wengine pia.

Huenda umekwishaazimia mambo mengi na makubwa ya kutekeleza ndani ya Mwaka huu 2020

Huenda umejiambia kwamba huu ndiyo mwaka wa kwenda kuanzisha biashara ambayo umekuwa unajiambia utaanzisha muda mrefu.

Huenda huu ndiyo mwaka ambao umepanga kuanza ujenzi wa nyumba yako.

Huenda huu ndiyo mwaka ambao umepanga kuingia kwenye ndoa au kama upo kwenye ndoa umepanga kuboresha mahusiano yako na mwenza wako na kuboresha maendeleo ndani ya familia yako

Na huenda huu ni mwaka ambao umejiahidi kubadilika!

Kuna mambo mengi ambayo umejiahidi kuyaacha mwaka 2019 na sasa umekuja 2020 ukiwa mtu mpya.

Kwanza nikupongeze sana kwa kufikiri na kupanga mambo hayo mazuri sana kwa mwaka huu mpya 2020.

Lakini nikupe tahadhari na kukukumbusha tu kwamba kila mwaka umekuwa unapanga mambo mengi na mazuri sana,

umekuwa unaweka malengo mazuri sana,

Lakini mwezi Januari unapoisha, wengi wetu tunakuwa tumeshasahau kabisa malengo hayo na kurudi kwenye maisha yetu ya kawaida.

Sasa ili mwaka huu 2020 uwe wa tofauti kwako na malengo yote uliyojiwekea uyafanyie kazi na kuyafikia, kuna jambo muhimu sana unatakiwa kulifanyia kazi kabla ya chochote!

Na hilo litawezekana kama tu utajiwekea lengo moja muhimu sana ambalo wengi huwa tunasahau kuliweka.

Lakini kabla ya kuingia kwenye lengo hilo muhimu ninalokushauri ujiwekee kwa mwaka huu mpya 2020, nikushirikishe kauli moja kutoka kwa aliyewahi kuwa raisi wa Marekani, Abraham Lincolin. Aliwahi kunukuliwa akisema;

"ukinipa masaa 6 ya kukata mti, nitatumia masaa 4 kunoa shoka langu".

Hiyo ni kauli fupi, lakini iliyobeba ujumbe mkubwa mno, ambao ukiuelewa, mwaka huu 2020 utakuwa bora na wa kipekee sana kwako.

Anachosema Lincolin ni kwamba kabla hujakimbilia kufanya kile unachotaka kufanya hakikisha kwanza una zana bora ya kufanya kitu hicho!

Kwenye kukata mti zana ni shoka, lakini kama shoka ni butu, utatumia muda mwingi na nguvu nyingi kukamilisha kazi hiyo na pengine unaweza kuchoka na kukata tamaa na ukashindwa kuendelea na kazi hiyo!

Lakini shoka likinolewa vizuri nguvu kidogo na muda mchache utatumika kukamilisha kazi.

Hivyo kama utaweka muda mwingi kwenye kunoa shoka, utakuwa na ufanisi zaidi kwenye kukata mti.

Na hilo ndilo lengo kuu mahususi unalotakiwa kuanza nalo ili uweze kufikia malengo yote uliyojiwekea 2020.

Tumia muda wako kunoa shoka lako ambalo ni akili yako! Ongeza maarifa kwenye jambo unalotaka kufanya! Tafuta ujuzi, tafuta maarifa mapya, tengeneza "time frame" ya lengo lako, yaweke kwa mpangilio malengo yako (scale of preference), kisha saka maarifa tena na tena kuhusu jambo hilo!

Unapokuwa na fikra sahihi, zinafanya uwe na mtazamo sahihi kitu ambacho kitapelekea uchukue hatua sahihi na kisha kupata matokeo bora.

Nimalizie kwa kusema, kabla ya kuanza kukata mti hakikisha kwanza kama shoka lako limenolewa vizuri! Kama utagundua haliko vizuri, rudi nyuma, noa shoka lako kisha ingia mzigoni ukiwa fiti na zana fiti!

HAPPY NEW YEAR 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nice one bro. Thanks for such an important advice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…