UNASEMAJE JUU YA KESI YA MAUWAJI YA 02/12/2018.

UNASEMAJE JUU YA KESI YA MAUWAJI YA 02/12/2018.

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
613
Reaction score
313
Ndani ya nyumba moja ilio na vyumba 4 ambavyo vinapangwishwa katika vyumba hivyo kimoja wanakaa mtu na hawara wake ambapo Mwanamke mwenye asili ya Tanga anasadikiwa kumuuu mwnaume wake huyo ingwawaje mwanamke huyo anasema kua mwanaume huyo amejitundika mwenyewe.

Ndani ya Choo ilikutikana maiti ambayo imewapa watu wasiwasi kua marehemu hakujinyonga bali aliuliwa kisha muili wake kuenda kutundikwa chooni na kusingiziwa kua marehemi amejitundika.

Muonekano wa mazingira ya kujitundikia ni kama haya yafuatayo:-

1. Mwili wa marehemu ulikutikana chooni ukinighinia kwa kutundikwa kwa kanga

2. Urefu wa kutoka katika sakafu hadi katika boriti ambayo inasadikiwa marehemu kujitundika ni futi 7 tu.

3. Marehemu alikua na urefu wa futi 5.5 ama sita kasoro kidogo.

4. Marehemu alikua uchi katika kitanzi hicho na bukta yake ilionekana chini karibu na sink la choo.

5. Mwili wa marehemu ulikua na tofauti ya nchi moja Baina ya magoti na sakafu ya choo

6. Vidole ya gumba vya miguu viligusa sakafu ya chooo

7. Maiti haikuonekana na kinyesi wala kipovu mdomoni


Jeeee wanasheria kwa hali hiii tunasemaje juuu ya hili tulio inawezekana kweli mtu kujinyonga wakati miguu yake inagusa chini?

Katika nyumba hio nani atakua mtuhumiwa wa tukio hilo?

Jeee u aweza kumshtaki mwanamke wake kwa kosa la kuumuuwa mwanaume wake?
 
Kwani si kuna post mortem ambayo inaweza kudetermine cause of death? Yani tuanze kuwanga hapa wakati kuna scientific methods?
 
Dalili ya kwanza ya kujua kama mtu kajinyonga lazima ukute mikono ilikua inaelekea shingoni kujinasua na kitanzi huo ndio huwa ushahidi wa kwanza wa kimazingira
 
Hata km itaonekana alinyongwa, bado JAMHURI ina wajibu wa kuthibitisha kuwa alinyongwa na yule mama au mpangaji anayedhaniwa. Haitoshi kusema kwa vile alikuwa anakaa na yule mama, bhasi ndiye alimnyonga.
 
Dalili ya kwanza ya kujua kama mtu kajinyonga lazima ukute mikono ilikua inaelekea shingoni kujinasua na kitanzi huo ndio huwa ushahidi wa kwanza wa kimazingira
Hili halikuonekana wengine wamefika mbali hadi kusema kua kitazi hakikukaza sana kwa kuonesha kua kilikaza kwa sababu ya kunighinia
 
?
fahamuzaidi-20181203-0001.jpeg
 
Kama hamjakuta nya kidogo iki chungulia pale uani nakapovu kamakile cha castle lite kidogo ndomoni na kisusio kidogo puani basi huyo hajajinyonga .
 
Back
Top Bottom