Unasemaje kuhusu kuokoka na wake zaidi ya mmoja?

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,156
Reaction score
1,667
Soma kwa makini sana,

Mtu ameshuhudiwa kumjua Mungu amekubali ameokoka na anawake wawili au watatu wote amewatolea mahari, kwao anatambulika na wake nao wamekubali kuokoka, wote wake zake na watoto wameokoka.

Kuna kitu watumishi na wengi waliookoka utasikia hapa, mmeokoka tayari cha kufanya wewe mwanaume inabidi uwaache wote uwe na mke mmoja wa kwako. Kweli Biblia insema usimuache mke wa ujana.

Ukiisoma vizuri unaambiwa,

Moja ~ Usihukumu usije ukaukumiwa.

Pili ~ Inasema yaache magugu na ngano vikue pamoja Bwana atavuna siku ya mwisho.

Tatu ~ Mungu anawajua walio wake.

Nne ~ Mbinguni hawaoi wala kuolewa.

Tano ~ Ukiisoma kwa mujibu wa amri za Mungu inasema, usizini, usitembee na mtu asiye mke wako au mume wako. Sasa huyu amewaoa na mahari ametoa anatambulika kote pamoja na jamii.

Sita ~ Sulemani alioa wake mia saba, Ibrahimu alizaa na mjakazi hajiri alikuwa anaishi naye japokuwa baadaye alimfukuza kwa kosa la kumkashifu mke wake Sara.

Saba ~ Ukiisoma mwanzo anasema enendeni ulimwenguni mkazaliane na kuujaza ulimwengu, na wengi wa hali hii wanashindwa kuokoka kutokana kuwa akiokoka tu ataambiwa awaache wake zake abaki na mmoja.

Wachungaji wengi wanakimbilia muachane ubaki na mmoja.
Kumbuka kazi ya mchungaji ni kukusanya kondoo siyo kutawanya na kuwafundisha wafike mbinguni.

Kumbuka Mungu huaangalia moyo wa mtu hata kuokoka ni yeye amemshawishi aokoke.

Mwisho kumbuka wanapendana, hawana ugomvu wowote na wanawatoto. Swali hili ni la msingi inapaswa tulijue,

Unasemaje kuhusiana na hili?
 
Tuanze na ww kwanza nini maana ya mke wa ujana?
 
Mk 10:6 SUV
Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.

Kwenye Maandiko, tunaanza muona Lameki kuwa na wake wengi Ada na Sila ( kama sijakosea), - tunaona source ya mtu kuwa na wake wengi ni upande ambao Mungu ali ulaani. Tunaenda tunakutana na Jakobo kuwa na wake wengi ( evil manipulation) tutamkuta Daudi na tuta mkuta Selemani..

Je? Nini ndoa.. Picha kamili tunaweza kuwa tumwipata
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Mke ni mmoja tu. Hivo mke wa kwanza ndiye wa kubaki nae ikiwa wokovu kampa Yesu. Ila kama kajipa aendelee nao Baba hana hasara. Akufinyange bado wew ulie vumbi umsumbue. No
 
Mk 10:6 SUV
Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.

Kwenye Maandiko, tunaanza muona Lameki kuwa na wake wengi Ada na Sila ( kama sijakosea), - tunaona source ya mtu kuwa na wake wengi ni upande ambao Mungu ali ulaani. Tunaenda tunakutana na Jakobo kuwa na wake wengi ( evil manipulation) tutamkuta Daudi na tuta mkuta Selemani..

Je? Nini ndoa.. Picha kamili tunaweza kuwa tumwipata
Hakyanani sijakuelewa🙄🙄🙄😴😴😰
 
Unaokoka ili uende wapi?
Mbingu ya wanadamu au ya Mungu?
Maana ukiwaacha hao wake zako utawapa masikitiko ya moyo.
Hivyo unakuwa umewatendesha dhambi.
Hakuna mbingu ya Mungu utaingia.
Ila ya wanadamu utaingia tu.
Maana ni unafiki kwa kwenda mbele
 
Hao wote ni wake zake halali hivyo anatakiwa kuendelea kuishi nao.

Anayetakiwa kuwa na mke mmoja ni yule ambaye amekoka akiwa hana mke, au ameokoka akiwa na mke mmoja tu. Lakini, hata yule ambaye ana mke zaidi ya mmoja hatakiwi kuongeza mke mwingine tena baada ya kuamini.

Mtume Paulo anapo andika waraka kwa Timotheo kuhusu sifa za askofu anasema inampasa askofu awe MUME WA MKE MMOJA hii inaonyesha possibly kwenye kanisa ambalo Timotheo alikuwa analisimamia kulikuwa na waumini ambao wako na mke zaidi ya mmoja (yaani waliingia ktk imani wakiwa tayari wameoa zaidi ya mke mmoja) ndio maana anaonyesha kwamba mtu aliyeamini lakini anamke zaidi ya mmoja hapaswi kupewa nafasi ya askofu, kwa sababu atakuwa na majukumu mengi ya familia na hivyo kushindwa kusimamia vema nafasi yake ya utumishi ktk kanisa.

Sasa ikiwa hata katika siku za Paulo mtume wa injili ya Yesu kwa mataifa hakufukuza watu ambao wameoa mke zaidi ya mmoja sisi tutoe wapi ujasiri wa kuleta kikwazo kwa watu walio mgeukia Mungu na Kristo wake eti kwa sababu tuu ameokoka akiwa na mke zaidi ya mmoja?.
 
Umejibu vyema, mkuu Kuna uzuri wa kujisomea biblia we mwenyewe kuliko kusomewa na Hawa viongozi wetu tu, biblia ni pana
 
Soma kwa makini sana,

Mtu ameshuhudiwa kumjua Mungu amekubali ameokoka na anawake wawili au watatu wote amewatolea mahari, kwao anatambulika na wake nao wamekubali kuokoka, wote wake zake na watoto wameokoka.

Kuna kitu watumishi na wengi waliookoka utasikia hapa, mmeokoka tayari cha kufanya wewe mwanaume inabidi uwaache wote uwe na mke mmoja wa kwako. Kweli Biblia insema usimuache mke wa ujana.

Ukiisoma vizuri unaambiwa,

Moja ~ Usihukumu usije ukaukumiwa.

Pili ~ Inasema yaache magugu na ngano vikue pamoja Bwana atavuna siku ya mwisho.

Tatu ~ Mungu anawajua walio wake.

Nne ~ Mbinguni hawaoi wala kuolewa.

Tano ~ Ukiisoma kwa mujibu wa amri za Mungu inasema, usizini, usitembee na mtu asiye mke wako au mume wako. Sasa huyu amewaoa na mahari ametoa anatambulika kote pamoja na jamii.

Sita ~ Sulemani alioa wake mia saba, Ibrahimu alizaa na mjakazi hajiri alikuwa anaishi naye japokuwa baadaye alimfukuza kwa kosa la kumkashifu mke wake Sara.

Saba ~ Ukiisoma mwanzo anasema enendeni ulimwenguni mkazaliane na kuujaza ulimwengu, na wengi wa hali hii wanashindwa kuokoka kutokana kuwa akiokoka tu ataambiwa awaache wake zake abaki na mmoja.

Wachungaji wengi wanakimbilia muachane ubaki na mmoja.
Kumbuka kazi ya mchungaji ni kukusanya kondoo siyo kutawanya na kuwafundisha wafike mbinguni.

Kumbuka Mungu huaangalia moyo wa mtu hata kuokoka ni yeye amemshawishi aokoke.

Mwisho kumbuka wanapendana, hawana ugomvu wowote na wanawatoto. Swali hili ni la msingi inapaswa tulijue,

Unasemaje kuhusiana na hili?

Duh.. hapa nangojea muongozo wa mama D

Mtu ana wake zake watano na ana furaha na amani na wake zake na mmeamua kumrudia Mungu unawaambia waachane!? Eti ili Mungu awakubalie na kuwahesabia haki!??

Kwa hiyo watoto waliozaliwaga ndani ya hiyo familia nao watupwe!? Au wanyongwe!?

Ukisikia uchawi ndio huo🙄🙄🙄

Mungu alimbariki Ishmael na hajri wewe ni nani useme watengane?

MWANZO 16: 5-11

5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.
6 Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.
7 Malaika wa Bwana akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.
8 Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.
9 Malaika wa Bwana akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.
10 Malaika wa Bwana akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
11 Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako.
 
Ni vizuri kuelewa kuwa Biblia iko kimya kwa mazingira ya mtu kuamua kuokoka na wake alikuwa nao kabla nao kuamua kuokoka.
Biblia imetaja mara kadhaa kuhusu mume au mke kuwa na mwenzi asiyeamini kama mistari hapa chini kama anavyoandika Paulo,na anaweka wazi kwa uzoefu wake.
Iko hivi,Yesu anasema mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru.
Kadri tunavyomfahamu Mungu zaidi ndio tunavyokuwa huru zaidi mpaka kwenye maamuzi sahihi ya hekima ya Kimungu.
Itoshe kusema hekima ya Mungu iko juu sana na njia zake hazichunguziki.
Kwa huyo ndugu ni suala la muda tu,kila kitu kitakaa sawa bila kuacha maswali kwa mtu yoyote,zaidi ya kusema hekima ya Mungu ni ya ajabu.
1 Wakorintho 7:10-16
[10]Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
[11]lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
[12]Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
[13]Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
[14]Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
[15]Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
[16]Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?
 
Mtu ana wake zake watano na ana furaha na amani na wake zake na mmeamua kumrudia Mungu unawaambia waachane!? Eti ili Mungu awakubalie na kuwahesabia haki!??

Kwa hiyo watoto waliozaliwaga ndani ya hiyo familia nao watupwe!? Au wanyongwe!?

Ukisikia uchawi ndio huo🙄🙄🙄

Mungu alimbariki Ishmael na hajri wewe ni nani useme watengane?

MWANZO 16: 5-11

5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.
6 Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.
7 Malaika wa Bwana akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.
8 Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.
9 Malaika wa Bwana akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.
10 Malaika wa Bwana akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
11 Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako.
Hi Mama D!
 
Enh hutaki kuacha mbususu mbili kati ya tatu, uko ni mke mmoja mme.mmoja si lazima uokoke na usibadili mitazamo yao wao wewe ni nani umewafata mwenyewe.

Back
Top Bottom