Unashauri nini kifanyike ili sekta ya afya iweze kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania?

Unashauri nini kifanyike ili sekta ya afya iweze kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania?

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
Je, wajua?

Serikali ya Tanzania chini ya Marais toka awamu ya kwanza hadi sasa awamu ya Sita imechukua hatua mbalimbali kuimarisha huduma za afya nchini kwa kujenga miundombinu ya afya.

Zikiwemo zahanati, vituo vya afya, hospital za halmashauri, hospital za wilaya, hospital za mkoa, hospital za rufaa ngazi ya mkoa, hospital za kanda na hospital za Taifa, uanzishaji wa taasisi za kibingwa (MOI, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Saratani Ocean Road nk) pamoja na ununuzi na usimikaji wa vifaa tiba,

Mitambo, mashine za uchunguzi za kisasa, ununuzi wa dawa aina zote, uanzisha wa mfumo bora wa ugharamiaji matibabu kupitia bima ya afya, taasisi za mafunzo na elimu juu ya masuala ya tiba na afya kwa ujumla, kuwekeza kwa wataalam wa tiba na afya lengo likiwa ni kuboresha huduma za msingi ili kuhakikisha watanzania wanapata matibabu bora, kwa uhakika, urahisi na kwa gharama nafuu.

Swali la Leo:

Kwa maoni yako, unadhani hatua gani nyingine zinaweza kuchukuliwa ili kuboresha zaidi sekta ya afya ili iweze kutoa huduma bora zaidi kwa kila mtanzania?

#AfyaKwanza
 
Viongozi waache kujipangia bajeti kubwa kwa matumizi ya anasa kama magari ya kifahari na kulipana mishahara na maposho makubwa kwao wao wenyewe na wenza wao kama walivyopitisha sheria hiyo ya kipuuzi hivi karibuni,
Pia waangalie miradi yenye tija kwa nchi,wafute mashirika yanayoendeshwa na ruzuku ya serikali huku yenyewe yakiendelea kupata hasara kila mwaka ili fedha zitakazookolewa ziende kwenye huduma za afya na gharama za matibabu zipungue kwa wananchi.
Ni kweli serikali imejitahidi kujenga miundombinu ya hospitali na kuweka vifaa tiba vya kisasa lakini watu wengi wanashindwa kumudu gharama za matibabu na ni wananchi wachache ndiyo wanafaidika na huo uwekezaji mkubwa wa serikali katika sekta ya afya.
Lakini pia wapunguze kwenda kufanya matibabu nje ya nchi kwa sababu hata huko malaika mtoa roho yupo na hivi karibuni wamerejesha wenzao wawili.
Kama wao wameridhishwa na hali ya huduma za afya hapa nchini huko nje wanafuata nini?
 
Back
Top Bottom