ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,154
- 4,184
Kama kawa kama sawa!!
Kila siku nasikia vijana mabachela wanauliza kuhusu hili swala la mke kuwa Wife material au kwa wadada kutafuta mwanaume husband material au kwa ufupi wanatafuta mtu ambaye ni family material.
Leo nidodose tu tunapozungumzia mtu kuwa family material tunamaanisha nini?
Kigezo cha kwanza ni uelewa na ukomavu.Hiki ni kigezo cha muhimu sana kwa wanando hasa kwa kuwa uwo uzuri wa sura unaenda ukichuja kadiri umri unavyoenda na uo uwezo wa kifedha unawezakupungua na hata mambo mengi yanaweza kubadili lakini personality ya mtu ni vigumu sana kubadilika ukiacha zile personality swings za kawaida ambazo ni kawaida kwa kila binadamu
Hivyo basi unapotafuta mke ambaye ni wife material jiulize kama wewe ni husband material!vile vile unapotafuta husband material jiulize kama wewe ni wife material kwa sababu ila mke na mume muweze kudumu pamoja lazima wote muwe family material.
Jambo jingine la muhimu la kutafakari ni kwamba,hatuoi kwa sababu ya ngono au kuzaa au kutunzana ingawa hayo ni mambo muhimu sana katika uhusiano.Unapoingia katika ndoa na mtu mwingine iwe ni kwa sababu unampenda,unamuelewa na unamjali kwani safari ya ndoa ina mambo mengi sana ambayo mtayavuka tu iwapo unampenda,unamuelewa na unamjali mwenzi wako
Ndoa sio utumwa wala mke sio mtumwa wa mume.Mke ni mwenza wa ridhaa yake mwenyewe na hata mume pia anapaswa kutambua hilo
Niwasihi wale waoaji jihadharini na ndoa za mwendo kasi!!hakikisha kwanza wewe mwenye uko tayari kuchukua jukumu hilo lakujenga familia kabla ya kuanza kutafuta mwanamke aliye tayari.Na unapompata usimkurupushe nenda naye taratibu.After all you have the whole life to see each other so no need to rush things.
Asubuhi njema