Watu uliofanya nao uzinzi, nafsi zao hubakia ndani yako kwa kazi maalum. Soma hii:
- Ili kututesa.
- Kuja katika ndoto, na kushiriki uzinzi na sisi.
- Kutuzuia tusioe au kuolewa.
- Kutuvurugia amani na upendo kwenye mahusiano mengine au ndoa.
- Kujichua kupitia nafsi zao.
- Kutufanya tuwe makahaba kwa kutamani kulala na kila mwanaume/mwanamke mpya mbele ya macho yetu.
Siku ya leo nitakupa mwongozo wa maombi utakao tumia kujitenga na kila nafsi ya mtu yeyote iliyo ndani yako inayozuia na kuharibu maisha yakoβusiingie kwenye ndoa, inayozuia usipate mahusiano na usiolewe wala kuoa, inayofanya uendelee na uzinzi na ukahaba, inayofanya ujichue mara kwa mara.
Kuna nafsi za watu wengi zinaishi ndani ya mtu kumtesa kulingana na watu aliowahi kushiriki nao uzinzi. Kila aliyeshiriki uzinzi na wewe, nafsi yake hubaki ndani yako kukutesa na wakati mwingine kukuzuia usipate mume/mke mwingine, ili abaki yeye tu katika ulimwengu wa roho.
Akiwa ni mwanaume mmoja, basi kunakuwa na nafsi moja.
Wakiwa ni wawili, basi kunakuwa na nafsi mbili.
Wakiwa watano, basi kunakuwa na nafsi tano zikishindanda ndani ya mtu, na mara nyingi zinamsumbua hata usiku kwa kumbukumbu za matukio, na mara nyingi zinamsumbua kwa kuja katika ndoto kushiriki naye tendo, n.k.
Leo tutajitenga nazo.
Kila unayemkumbuka, jitenge naye.
Kata mawasiliano.
Kataa nafsi yake inayoishi ndani yako.
Kataa ile roho (spirit) inayoishi kwako.
Simamia hii mistari, soma kwa umakini:
- Mithali 3:32β33
- 1 Wakorinto 6:15β19
Nafsi zetu zikishashiriki uzinzi tu, zinakuwa chafu kwa kushambuliwa na kila adui wa kuzimu, wakidhania tumeshaungwa nao kuwa kitu kimoja. Zinakuja ndani yetu kutaka ushirika, maana zilikuwa na ushirika na fulani uliyelala naye.
Wakati mwingine, kama wale ulio lala nao walikuwa na nafsi zinazoishi ndani yao, basi unapolala nao, zile nafsi pia huja ndani yako. Ukiunganisha na ya kwake, basi linakuwa jeshi kubwa.
Ushuhuda:
Rafiki mmoja alikuwa na mahusiano na binti mmoja, walilala pamoja sana na kushiriki uchafu... Itaendelea.