Unataka Kufanya Biashara?

mjasiria

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Posts
4,156
Reaction score
1,862
Habari wanaJF? Nina imani tunaendelea vyema katika kutafuta mafuta ya kulainishia vyuma. Niende moja kwa moja kwenye mada.

Kama unasoma hapa nina uhakika sio mara moja au mbili umejiuliza biashara gani ukiafanya itakulipa. Wengine tunajiuliza ni biashara ipi ina njia za mkato kufikia lengo la kuwa na pesa. Kuondokana na pesa za mawazo, mtu unaamka asubuhi badala ya kusoma gazeti na kupitia taarifa zako za kifedha wakati huo ukipata kifungua kinywa murua kabisa, unajikuta unawaza mkopo wa benki na deni la dukani kwa Mangi mtaa wa pili. Hakuna anayependa kuishi haya maisha ila ndiyo hivyo vyuma vinakaza kwelikweli.

Pamoja maumivu yote bado kuna njia na kanuni ambazo zikifuatwa vizuri na kama kudra ipo, zinakupatia matokeo chanya. Sisi wengine tunaamini jitihada haishindi kudra ila hii haina maana usifanye jitihada. Sasa basi tukirudi kwenye swali letu, ni biashara gani inalipa leo hii? Jibu ni zote. Kwa nini nasema hivi? Ni kwa sababu uzuri au ubaya wa biashara unategemea na mambo yafuatayo hapa chini.
  1. Utayari na ujuzi wa biashara husika. Kwa mfano, kama unataka kufanya biashara ya samaki ni vizuri ujitahidi kujua mambo mengi kwa kadri uwezavyo kuhusu samaki, upatakanaji wake, msimu wake, changamoto zake ikiwamo usafiri, kodi, mamlaka zinazohusika na mbinu nyingine ambazo zinaweza zisiwe rasmi ambazo hutumika katika biashara ya samaki.
  2. Maarifa sahihi ya upatikanaji wa soko la bidhaa husika. Kwa mfano haitoshi tu kujua bei ya samaki mahali wanakonunuliwa na bei ya kuuzia sokoni. Kama ukiweza kuwa mdadisi ujue samaki wanatokaje kwenye soko husika, kwa mfano je soko unalotarajia kuuza wanatoka zaidi changu au kolekole? Ushuru na kodi wanafanyaje? Kuna vibali vyovyote ambavyo inabidi uwe navyo?. Jiulize kama unaweza kuingia katika soko na kuleta ushindani wa kutosha kiasi cha kusimamisha biashara yako. Unaweza kuamua kwenda kwenye soko la samaki hata wiki nzima unajifunza kwa kutazama tu hata wiki nzima, na wakati huohuo fanya urafiki na baadhi ya wauza samaki hapo sokoni, kuna watu sio wachoyo watakupa maarifa ya kutosha tu.
  3. Usifikirie mahitaji ya biashara yako kama vile ishakuwa kubwa wakati ndiyo unaanza. Hapa nazungumzia biashara ya kawaida kabisa. Kwa mfano tukiendelea na habari ya samaki ingawa naona kama wameshaanza kujazo shombo kwenye posti ila tuvumiliane tu hivyohivyo - jiulize ni vitu gani unahitaji kwa kiwango cha chini ili uanze baishara yako? Usifikirie friji, mzigo mkubwa wa kuanza nao na mambo mengine makubwa makubwa, angalia aina ya soko unaloingia kuliko kiwango cha mtaji ulichonacho.
  4. Angalia washindani wako wanafanya nini ili wewe utengeneze kitu bora kuliko wao. Kama unataka kuuza samaki unaweza hata kuboresha namna unavyofunga tu samaki wako, lakini kuwa makini na gharama.
  5. Kuna namna yeyote unaweza kufanya promosheni - najua hili ni changamoto ila hakuna kinachoshindikana kama unaweza jaribu kufanya kuwa mbunifu na ufanye promosheni. Kubali kupata faida ndogo ili kadri siku zinavyoenda mzigo utoke mkubwa hivyo kukuongezea wewe faida.
  6. Angalia namna ya kudili na maadui zako hata kabla hawajatokea. Hii nitaomba tuchangie mawazo wote maana maadui wanategemea sana na aina ya mazingira unayofanyia biashara.
  7. Usione aibu kuwa tofauti na wengine na pia usitegemee ndumba.
  8. Angalia mtaji sasa na mahali unakoweza kuupata. Kama inabidi uhifadhi kidogokidogo hadi ufike fanya hivyo. Kama utakopa fanya hivyo ila binafsi sishauri ukope mtaji wote kuanzisha biashara, jitahidi angalau 50% itoke mfukoni mwako isipokuwa kama unataka kufanya biashara za ujanja ujanja, hapo unaweza kuanza na mtaji wa blah blah tu inatosha.
Haya wakuu wenye madini zaidi tumwagike kwenye comments tuendelee kuelimishana zaidi na zaidi kuhusu mbinu mbalimbali za kuleta mlainisho wa vyuma na mambo mengine.
 
Safi sana mkuu wabongo wengi huwa tunafeli kwenye tafiti tu.Huwa hatuwazi kufanya tafiti kwanza ndo maana biashara nyingi zinafeli,mtu akiambiwa hichi kinalipa anaingia mzima mzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…