UNATAKA KUNUNUA GARI UK? Serengeti freight tuko kwa ajili yako

UNATAKA KUNUNUA GARI UK? Serengeti freight tuko kwa ajili yako

Chris Lukosi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
4,583
Reaction score
2,944
SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD

WAZEE WA KAZI

GOOD NEWS FOR ALL
UNATAKA KUNUNUA GARI UK?
USIUMIZE KICHWA
CHAGUA GARI SEHEMU YOYOTE UK HALAFU TUTUME SISI TUKALIKAGUE
USINUNUE GARI BILA KUKAGULIWA
USINUNUE PICHA YA GARI AU CHETI CHA UKAGUZI
TUNATOA HUDUMA YA UKAGUZI WA MAGARI KWA KUTUMIA AUTOMATIC TEST LANES, MITAMBO MIPYA YA KISASA ILIYOPASISHWA NA VOSA. UKICHAGUA GARI KWENYE MTANDAO TUTUMIE DETAILS SISI TUTATUMA WAKAGUZI WETU WANAOTAMBULIWA NA VOSA KWENDA KULIKAGUA GARI ULILOCHAGUA KUHAKIKISHA KUWA UNANUNUA GARI LA UHAKIKA NA SIYO MATATIZO.
TUNAKAGUA UBORA WA GARI (ENGINE &BODY)
TUNAKAGUA UHALALI WA GARI (USIJE KUUZIWA GARI LA WIZI AU LA MKOPO)
TUNAKAGUA UHALALI WA MUUZAJI (WENGINE NI MATAPELI)
NA TUNAKAGUA KAMA KUNA UBOVU ULIOJIFICHA (DIAGNOSTICS)
WATU WENGI WAMEUMIA BAADA YA KUUZIWA MAGARI MABOVU YASIYO NA VIWANGO KWENYE MITANDAO NA WENGINE KUIBIWA. USINUNUE GARI KAMA HALIJAKAGULIWA KWANI UNAWEZA KUWA UNAUZIWA PICHA TU.
saxon_atl_bay_v-low_res.jpg

TUNACHUKUA DHAMANA HII KUHAKIKISHA UNANUNUA GARI LITAKAL;OKULETEA HESHIMA NA FURAHA SIO STRESS!

kama unataka kuagiza kitu au kufanya booking yoyote ingia kwenye website yetu au tupigie kwenye namba zifuatazo;

CHRIS LUKOSI +44 07903828119 & 07404279633
SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
HQ - UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
email: info@serengetifreight.co.uk or serengetifreight@yahoo.co.uk

Tell (+44) 01375 855917 Fax (+44) 01708202477
www.serengetifreight.co.uK
 
Kama tenda ushaipata sasa akili itatulia na hutakubali kutumika tena. Nimeamini kuwa mtaka cha uvunguni sharti ainame au ule usemi mtumikie Kafiri upate mradi wako.
 
Kama tenda ushaipata sasa akili itatulia na hutakubali kutumika tena. Nimeamini kuwa mtaka cha uvunguni sharti ainame au ule usemi mtumikie Kafiri upate mradi wako.
Endeleza majungu wenzako wanafanya kazi, ndio maana wengi wenu mnaishia kushikishwa mic.
 
Endeleza majungu wenzako wanafanya kazi, ndio maana wengi wenu mnaishia kushikishwa mic.

He he he! Acha hasira weye! Sie wengine tunapiga kazi mwanzo mwisho bila kujipendekeza na maisha yako bomba tuu.
Kama kushika mic hayo mnayo nyie mnaosujudia wanaume wenzenu ili mpatiwe mshiko au tenda. Mtu mzima ukiona anafanya mambo ambayo hata yeye moyo wake hauamini hilo jambo ujue ana kasoro. Wenzake hawa hapa nao wasubiri mchongo;
ImageUploadedByJamiiForums1367412990.088591.jpg
View attachment 92130
 
Hii ndio ishara ya kufilisika maana CCM wameshindwa kukutekelezeeni ahadi walizokupeni haaaa haaa haaa
 
Salaam,

Nimesoma kwa kina na kuelewa kilichoandikwa.

Nawezaje kuthibitisha "Legality" ya hiyo firm yenu.Nitashukuru nikipata namna ya kuverify hiyo kwakuwa kwa kufanya hivyo kutaweka uhakika wa mtu kuamua kutumia huduma hiyo.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
ningeamini zaidi kama kungekuwa na ofisi hapa tanzania.. na iwe registered, in any case i see ur office physicaly!!
 
Hi there
Unaweza kuingia hapa chini
Company Check - Free company financial check on SERENGETI FREIGHT FORWADERS LTD. Registered number 07382666. Free company accounts. Companies House information
 
ningeamini zaidi kama kungekuwa na ofisi hapa tanzania.. na iwe registered, in any case i see ur office physicaly!!
Ofisi tunayo Tanzania na iko registered
No 4 Magomeni mtaa wa mwinyimkuu
Sisi hatuhitaji utulipe sisi kukununulia gari, sisi tutakufanyia ukaguzi wa gari lako na kukushauri kama liko sawa halafu tunakuachia wewe upatane bei na muuzaji na kumlipa
Kazi yetu ni kuhakikisha unauziwa kitu unachokitaka sio picha, wazungu siku hizi wamekuwa wajanja sana na wamewapiga watu wengi tu
 
Sasa kaka nikitaka nyie ndio muninunulie as in niwatumie hela nyie inakuaje hapo?
 
Baada ya kuona posts zako humu, nitasita sana kufanya shughuli zozote na kampuni hii.
 
Baada ya kuona posts zako humu, nitasita sana kufanya shughuli zozote na kampuni hii.

Hata iweje siwezi kufanya biashara na wewe chris lukosi. Nyie magamba hamuaminiki. Kama mliweza kukwapua ela za BOT mchana kweupe ndio mtashindwa kunizulumu ka gari kangu?

Pia, nitaakikisha naweka post humu kuwajulisha wana bodi kuacha kufanya biashara na wewe. Alafu nashangaa sana, kwa nini usiende pale lumumba kutangaza hii biashara yako? Mimi sifanyi biashara na mtu mnafiki...
 
Ofisi tunayo Tanzania na iko registered
No 4 Magomeni mtaa wa mwinyimkuu
Sisi hatuhitaji utulipe sisi kukununulia gari, sisi tutakufanyia ukaguzi wa gari lako na kukushauri kama liko sawa halafu tunakuachia wewe upatane bei na muuzaji na kumlipa
Kazi yetu ni kuhakikisha unauziwa kitu unachokitaka sio picha, wazungu siku hizi wamekuwa wajanja sana na wamewapiga watu wengi tu

umeesikika kaka
 
KWENDA KULIKAGUA GARI ULILOCHAGUA KUHAKIKISHA KUWA UNANUNUA GARI LA UHAKIKA NA SIYO MATATIZO.
TUNAKAGUA UBORA WA GARI (ENGINE
&BODY)
NA TUNAKAGUA KAMA KUNA UBOVU ULIOJIFICHA (DIAGNOSTICS)
WATU WENGI WAMEUMIA BAADA YA KUUZIWA MAGARI MABOVU YASIYO NA VIWANGO KWENYE MITANDAO NA WENGINE KUIBIWA. USINUNUE GARI KAMA HALIJAKAGULIWA KWANI UNAWEZA KUWA UNAUZIWA PICHA TU.

Mkuu Lukozi. Hakuna machine au mitambo ambayo inaweza kukufahamisha kuwa engine ya gari kama ina ubovu uliojificha. Magari mengi tu unanuna na kucheki na hayakupi error codes zozote na ukiendesha baada ya cku mbili tatu engine inakufa au gearbox. Ununuzi wa magari ni gamble na hata mafundi wakongwe hawawezi kutabiri uzuri au ubovu wa engine kwa kuisikilza au kutumia mitambo unayosema.

Kwa ushauri hapo kwenye nyekundu ubadilishe maneno ama sivyo utajiingiza kwenye matatizo ..watu watanunua magari via wewe na yakiharibika utapata lawama sana. Mnaweza kusema mtakaguwa magari kuona ni mazuri na paperwork zote zilizo sawa. Walio wengi kwenye biashara hii huwa wanatoa warranty ya miezi 3, 6 hadi mwaka (parts and labour) ila kwa nyumbani hii ni ngumu... . Ni mtazamo wangu
 
Hata iweje siwezi kufanya biashara na wewe chris lukosi. Nyie magamba hamuaminiki. Kama mliweza kukwapua ela za BOT mchana kweupe ndio mtashindwa kunizulumu ka gari kangu?

Pia, nitaakikisha naweka post humu kuwajulisha wana bodi kuacha kufanya biashara na wewe. Alafu nashangaa sana, kwa nini usiende pale lumumba kutangaza hii biashara yako? Mimi sifanyi biashara na mtu mnafiki...

kaka kuna nini hapo mbona umekuja mbogo ? Me sijaelewa bado
 
kaka kuna nini hapo mbona umekuja mbogo ? Me sijaelewa bado
Hajaja mbogo,
Anawaeleza Ukweli. Kwanza kitendo cha huyu Lukos kua tu ni Gamba tayari imani ishanitoka maana hawaaminiki hawa!!
 
Back
Top Bottom