Unataka mtanzania awe mzalendo waikato anashuhudia uvunjifu wa katiba hadharani

Unataka mtanzania awe mzalendo waikato anashuhudia uvunjifu wa katiba hadharani

Peasant educator

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2020
Posts
209
Reaction score
187
Habari,
Nimekuwa nikitoa tahadhari ya kuja kuwa na mtafaruku ndani ya nchi na ikiwezekana vita vya ndani. Kwa sasa kumetamalaki kwa uvunjivu wa katiba yet hasahasa kwa viongozi wetu wa juu pamoja na wakuu wa nchi akiwemo SPIKA wa bunge na hata RAISI mwenyewe. Hao viongozi wengine ndo hawasemeki pamoja na kutoa matamko ya ovyo na kejeli wakiongozwa na dr. MN.

Viongozi wetu mnapotupeleka sio kwema, kama mmesoma historia basi mnajua wazi kabisa kuwa mnatupeleka vitani. Itafika siku woga utaisha kwa watu na wataeka maslahi yao pembeni na kuweka maslah ya taifa mbele. Tipping point inakaribia naomba mjue kusoma alama za nyakati.

Hivi sasa suala la uzalendo limekuwa adimu ila kama viongozi jiulizeni kwa nini imekuwa hivi? Na je viongozi wakubwa kuvunja katiba na sheria inajenga au kuvunja uzalendo? Taifa linalopelekwa bila ya katiba na sheria linajenga uzalendo kwa watu wake? Mwisho watu haohao mnaowakandamiza watakaa chini kuvumilia mpaka lini? Kama haki hamna haki wataitolea wapi? HUO NI MWANZO WA VITA!!! ITS JUST A MATTER OF TIME KUIFANYA NCHI IWE SOMALI NA MSUMBIJI!!!

Vita vya Uganda havikupiganiwa ndani ya nchi na Athari yake mpaka leo inaonekana kwa kuwa na uchumi mbovu pamoja na nyenginezo. Nyenginezo ni miaka ya 70 na 80 nadhani mlokuwepo na miaka kuanzia 7-9 mnakumbuka kilitokea nini? Viwanda vyeti kufa na mpaka leo kushindwa kuvihuisha kisa ni nini?
NAOMBA MTAFAKARI TENA NA MWENENDO WENU HUU!?

Kumbukeni watu walitoa wapi ujasiri wa kupigana na wazungu,wajerumani na vita tunavokejeliwa vya majimaji war na vyenginevyo na walikw tayari kufa kwa ajili ya nchi yao? Sisi hatuna arsenal km zao !na kipindi hiko wao walikw vizuri sana na watu walipigana!

Hii ni indhari tu lkn tunapoenda sio kwema ni kama vile tumetoka kwenye ukoloni wa wazungu kuja kutawaliana wenyewe sasa,wenye nguvu na madaraka wanaonea wanyonge ila wanyonge wakichoka mjue ata mtoe vifaru vyote kitanuka hapa. Na hicho kitu hakitakuwa kizuri kwa taifa letu! Tuangalie Myanmar huko sasahiv na tuache hivi vitu unnecessary mana tunaondoa kabisa uzalendo kwa watu wetu na kuwaondolea imani na viongozi wao! sheria na katiba yao! na mahakama zetu na ndo mana matokeo ya kuuana yamezidi sasahiv! Kumpeleka mtu mahakamani ni kupoteza mda tu(jedi ya kijinga tu miaka 2-5) mana haki hamna na ikija inachelewa kama utapata, watu wanaona bora wamalizane mitaani na hii ni kitu mbaya kwa taifa!!? Uhalifu umetamalaki tutafakari kwa nini????
 
Back
Top Bottom