Elections 2010 Unataka Prof. Baregu kugombea URAIS mwaka 2010? Jiandikishe hapa.

Elections 2010 Unataka Prof. Baregu kugombea URAIS mwaka 2010? Jiandikishe hapa.

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Posts
11,584
Reaction score
6,136
Baada ya Dr. Slaa kukaa kimya nimeona heri tumpe suport huyu ambaye anasema anafikiria kugombea. Haitakuwa mbaya sana tukimuonyesha moyo wa kuwa na imani na yeye baada ya kuvunjwa imani na CCM kwa miaka mingi.

Kwa waliofundishwa na huyu jamaa, wanamfahamu kwa karibu.

Pia kuipa chama cha CCM kuwa na RAIS na WABUNGE WENGI, ni sawa na kuipa CCM muuwaji na mchimba kaburi. Watatuuwa na kutuzima na tusahaulike MILELE.

Naanza tena mwenyewe kujiandikisha. Kama Mkandara utaona nikurudishe tena kwenye namba moja basi ntafanya hivyo.....

1.Sikonge 2.
 
mgombea wa chadema mwaka huu naona hata vichwa vinauma, but I still stand on Dr. Slaa.
 
Luteni,
Ile ya Dr. Slaa kugombea nimeomba Mods waifunge kabisa kwa sasa na labda ifufuliwe kama Dr. Slaa atabadili mawazo mwenyewe.

Kwa sasa hivi ni Prof. Baregu anajitokeza. Kama tukionyesha tuko makini katika kumpa NGUVU zaidi, basi itakuwa wazo zuri sana yeye kugombea kwa ticket ya CHADEMA na uzuri ni kuwa hata akikosa, basi hakuna kilichoharibika. Atarudi kushika chaki Chuo Kikuu chochote duniani.

Mabadiliko lazima tuyafanye wenyewe. Kama tukikaa na kulialia na kukubali CCM ituwekee mtu wanayemkataka wao, mhhhhh!!!!!!
 
Mimi simjui huyu Prof na sijasikia vitu alivyovifanya hata michango kupitia publications zake. Ninashindwa kuunga mkono wala kupinga labda apigiwe debe kwanza. Hata Obama alionekana kwenye seneti kwanza.
 
Luteni,
Ile ya Dr. Slaa kugombea nimeomba Mods waifunge kabisa kwa sasa na labda ifufuliwe kama Dr. Slaa atabadili mawazo mwenyewe.

Kwa sasa hivi ni Prof. Baregu anajitokeza. Kama tukionyesha tuko makini katika kumpa NGUVU zaidi, basi itakuwa wazo zuri sana yeye kugombea kwa ticket ya CHADEMA na uzuri ni kuwa hata akikosa, basi hakuna kilichoharibika. Atarudi kushika chaki Chuo Kikuu chochote duniani.

Mabadiliko lazima tuyafanye wenyewe. Kama tukikaa na kulialia na kukubali CCM ituwekee mtu wanayemkataka wao, mhhhhh!!!!!!
Mkuu Sikonge kwa hili tuko pamoja niliwahi kuanzisha thread ya Baregu for President nimeitafuta siioni, ila akiamua kuchukua fomu litakuwa jambo zuri sana maana ni maeneo yake ya kujidai ana uwezo wa kujenga hoja na kuisimamia, tatizo litakuwa kumuuza kwa wananchi wa chini hasa vijijini.
 
Unfortunately I am not moved. Sampulli ya Profesa Baregu kwangu haina tofauti na sampuli za akina Profesa Malima, Profesa Kapuya, Profesa Magembe, Profesa Msola, ... profesa...., ..., ...prof.... ..; ninawajua sana watu wa aina hiyo.

Post za juu kisiasa zinahitaji uwezo katika mambo mengine zaidi ya intellectual capacity ya mtu. Professor Baregu ni exceptionally intellectual na anaweza kuwa mshauri na mchambuzi mzuri sana, lakini siamini kuwa anaweza pia kuwa kiongozi mzuri katika ngazi ya Rais.

Dr Slaa alikuwa ni candidate mzuri sana lakini kwa vile mwenyewe kasita, huenda anajijua kuwa hayawezi. Kikwete alitamba sana wakati akiwa wazir akijiamini kuwa atafanya vizuri sana lakini leo tunajionea. Nbnakubaliana kabisa namaneno ya Nyerere kuwa Kasri lile linahitaji mtu mweye kichwa na moyo wenye pembe nne zikitzama pande zote nne za dunia, siyo kimojawapo tu. Unfortunately hatujapata mtu wa namna hiyo.
 
Nathani anaweza kuleta mabadiliko kutokana na ujasiri aliokuwa nao hata kufukuzwa Udsm
 
Kichuguu, nafikiri humtendei haki Baregu.

Hata mie kusema ukweli simfahamu zaidi ya kusoma habari zake.

Ila tofauti moja kubwa inayoonekana waziwazi hata kwa asiye na macho ni kuwa:

Wenzake wote wamenunuliwa na chama tawala kwa njia moja au nyingine. Angelikuwa na hamu ya kuganga njaa basi angelijiingiza CCM na si ajabu leo hii na yeye angelikuwa au Mkuu wa chuo fulani au shirika kama siyo Waziri.

Sasa mtu kama Kaka Kapuya, unashindwa kufahamu kama ni Mjasirimali au Waziri. Huku bendi ya mziki, huku machimbo ya dhahabu, huku hoteli, huku....................

Nafikiri hadi hivi sasa, Maprofesa na Ma Dr wote walio na hamu ya kupata pesa za harakaharaka basi wameshajiunga CCM na wanafaidi hela za Watanzania. Kwa walioshindwa au kutokutaka, basi wamejikalia pembeni wakiangalia.

Inawezekana asiwe ALMASI kwa leo ila akiwa na Bunge la CCM, moto utawaka.

Vinginevyo basi TUFURAHIE siku Muungwana atapewa miaka 5 mingine.
 
Tapika tu halafu ule tena Matapishi yako.

Hebu kwanza ona hiyo AVATAR yako, inaonyesha tayari urefu wa akili yako.

Hapo sitaki kujua Kikwapa chako sijui kinatoka perfume gani?

Umesoma kwenye heading bado wafungua na mwisho kuweka comment, msula eve.

Na wewe nawe na wish list zako..aaarrgghhh
 
Mwanakijiji,

Sasa hivi Tanzania imechanganya URAFIKI na UONGOZI. Kufa hatujafa ila cha moto tunakiona.

Sidhani kama akija Baregu kama Rais na CCM ikiwa na bunge (sidhani kama hili litabadilika) basi nchi itawaka moto.

Sintajali Rais awe nani. Kwangu mie ni kuleta Kiongozi wa upinzania kweli ili kulipa Bunge Msukosuko.

Labda hatimaye watafahamu BUNGE na wao kama WAGUNGE ni NINI kwa nchi ya TANZANIA.
Mara wakianza kuburuzwa, wataanza kusoma sheria zao na kufahamu uwezo wao.
Mahakama pia itabidi iwe hivyohivyo. Kwa mtindo wa sasa, hatufiki mbali.
 
wakati nwingine napata shida sana na jinsi tunavyo dhani kuhusu kiongozi bora, hii habari ya fulani anafaa mara filani. urais si mchezo inataka utashi wa mtu mwenyewe binafsi wala si elimu tu au makongamano yake
 
Luteni, hii linki ya hii shule ya globalization aliyotoa prof. haifunguki kwangu, unaweza kuiwaeka kama PDF? nataka kuicheck maana niko kwenye shule fulani kama hiyo.
 
Luteni, hii linki ya hii shule ya globalization aliyotoa prof. haifunguki kwangu, unaweza kuiwaeka kama PDF? nataka kuicheck maana niko kwenye shule fulani kama hiyo.

Mdau,

Hiyo kitu ipo kwene video sasa sijui labda tukusaidie kudownload tuiweke kama atachment kama itatosha.
 
Unfortunately I am not moved. Sampulli ya Profesa Baregu kwangu haina tofauti na sampuli za akina Profesa Malima, Profesa Kapuya, Profesa Magembe, Profesa Msola, ... profesa...., ..., ...prof.... ..; ninawajua sana watu wa aina hiyo.

Post za juu kisiasa zinahitaji uwezo katika mambo mengine zaidi ya intellectual capacity ya mtu. Professor Baregu ni exceptionally intellectual na anaweza kuwa mshauri na mchambuzi mzuri sana, lakini siamini kuwa anaweza pia kuwa kiongozi mzuri katika ngazi ya Rais.

Dr Slaa alikuwa ni candidate mzuri sana lakini kwa vile mwenyewe kasita, huenda anajijua kuwa hayawezi. Kikwete alitamba sana wakati akiwa wazir akijiamini kuwa atafanya vizuri sana lakini leo tunajionea. Nbnakubaliana kabisa namaneno ya Nyerere kuwa Kasri lile linahitaji mtu mweye kichwa na moyo wenye pembe nne zikitzama pande zote nne za dunia, siyo kimojawapo tu. Unfortunately hatujapata mtu wa namna hiyo.

Prof. Baregu ni bora mara million moja kuliko Kikwete.
 
Luteni, hii linki ya hii shule ya globalization aliyotoa prof. haifunguki kwangu, unaweza kuiwaeka kama PDF? nataka kuicheck maana niko kwenye shule fulani kama hiyo.
Jaribu ku Google moja kwa moja kwenye Youtube halafu search Baregu in Globalisation nafikiri unaweza kumpata vizuri tu.
 
Back
Top Bottom