Mkuu Sikonge kwa hili tuko pamoja niliwahi kuanzisha thread ya Baregu for President nimeitafuta siioni, ila akiamua kuchukua fomu litakuwa jambo zuri sana maana ni maeneo yake ya kujidai ana uwezo wa kujenga hoja na kuisimamia, tatizo litakuwa kumuuza kwa wananchi wa chini hasa vijijini.Luteni,
Ile ya Dr. Slaa kugombea nimeomba Mods waifunge kabisa kwa sasa na labda ifufuliwe kama Dr. Slaa atabadili mawazo mwenyewe.
Kwa sasa hivi ni Prof. Baregu anajitokeza. Kama tukionyesha tuko makini katika kumpa NGUVU zaidi, basi itakuwa wazo zuri sana yeye kugombea kwa ticket ya CHADEMA na uzuri ni kuwa hata akikosa, basi hakuna kilichoharibika. Atarudi kushika chaki Chuo Kikuu chochote duniani.
Mabadiliko lazima tuyafanye wenyewe. Kama tukikaa na kulialia na kukubali CCM ituwekee mtu wanayemkataka wao, mhhhhh!!!!!!
Na wewe nawe na wish list zako..aaarrgghhh
Luteni, hii linki ya hii shule ya globalization aliyotoa prof. haifunguki kwangu, unaweza kuiwaeka kama PDF? nataka kuicheck maana niko kwenye shule fulani kama hiyo.
Unfortunately I am not moved. Sampulli ya Profesa Baregu kwangu haina tofauti na sampuli za akina Profesa Malima, Profesa Kapuya, Profesa Magembe, Profesa Msola, ... profesa...., ..., ...prof.... ..; ninawajua sana watu wa aina hiyo.
Post za juu kisiasa zinahitaji uwezo katika mambo mengine zaidi ya intellectual capacity ya mtu. Professor Baregu ni exceptionally intellectual na anaweza kuwa mshauri na mchambuzi mzuri sana, lakini siamini kuwa anaweza pia kuwa kiongozi mzuri katika ngazi ya Rais.
Dr Slaa alikuwa ni candidate mzuri sana lakini kwa vile mwenyewe kasita, huenda anajijua kuwa hayawezi. Kikwete alitamba sana wakati akiwa wazir akijiamini kuwa atafanya vizuri sana lakini leo tunajionea. Nbnakubaliana kabisa namaneno ya Nyerere kuwa Kasri lile linahitaji mtu mweye kichwa na moyo wenye pembe nne zikitzama pande zote nne za dunia, siyo kimojawapo tu. Unfortunately hatujapata mtu wa namna hiyo.
Jaribu ku Google moja kwa moja kwenye Youtube halafu search Baregu in Globalisation nafikiri unaweza kumpata vizuri tu.Luteni, hii linki ya hii shule ya globalization aliyotoa prof. haifunguki kwangu, unaweza kuiwaeka kama PDF? nataka kuicheck maana niko kwenye shule fulani kama hiyo.