Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

Unataka Wowowona Hips?
 
Partner wa ku jog weekend hii kutoka Makonde hadi beach komba
 
Nilinunua elfu 10, ukiwa Feri unataka kuvuka kwenda kigamboni utakuta kuna jamaa ameweka vitu vya mazoezi na hivyo vitairi anavyo.

Kula ni kawaida ila isiwe junk food (Burger, Pizza n.k)
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Mazoezi ukiyazoea inakuwa ni kama starehe. Nilianza kuota kitambi mara tu nilipopata kiajira na kuanza kuzikunja noti na kubahatika kupata kausafiri kakutembelea, nikaona sasa huko ninapoelekea nitapasuka. Nikiangalia muda wa kufanya mazoezi nakosa kabisa, naingia kazini asubuhi narudi jioni. Nikaona chakufanya hapa ni kuamka alfajiri nifanye mazoezi ndio niende kazini. Nikaanza kuamka saa 11:00 alfajiri kila siku, naenda uwanjani kukimbia kuzunguka uwanja. Siku ya kwanza nilizunguka mara 6, siku zilivyozidi kwenda nikawa naongeza, hatimaye nikawa naweza kuzunguka mara 35, na nikitoka kukimbia nikifika home nafanya mazoezi ya tumbo kama crunches, sit ups, n,k.

Siku hizi nimebadili utaratibu, sihesabu tena mizunguko ninayozunguka uwanja bali nakimbia kwa saa 1 bila kupumzika. Kitambi kimeyeyuka na nina six-pack, najisikia vizuri muda wote, nimechangamka na ninajiamini. Nimezoea kufanya mazoezi hadi nikikosa kufanya nahisi kupungukiwa kitu kwa siku hiyo.

Ukichukulia mazoezi ni adhabu, utafanya kwa siku chache na kuacha. Mazoezi ni matamu asikwambie mtu. Tufanye mazoezi wakuu.

Nimeona nishee hii ili wengine nao wahamasike
 
Nikiwa nafanya mazoezi hua nasikiliza wimbo upo kwenye filamu za Rocky (Rocky Balboa theme song) unaitwa Gonna Fly Now, hua unanitia moyo sana.
Pick yours fast....
 


Share hiyo diet plan yako mkuu, tupo wengi tunaotamani kukata futa
 
Share hiyo diet plan yako mkuu, tupo wengi tunaotamani kukata futa

 
Ukianza mazoezi iwe ndio kama kilevi chako,sio eti baada ya kupungua uache UTAKUWA BONGE AFADHARI YA MWANZO,NA WATU WENGI HAWALIONGEI HILI. WAANGALIE WANAMICHEZO WOTE WALIOACHA AU KUPUNGUZA MAZOEZI WANAVYOKUWA.
Refer Louis Nazario De Lima ( Ronaldo)

Ukianza mazoezi iwe ndio kama kilevi chako,sio eti baada ya kupungua uache UTAKUWA BONGE AFADHARI YA MWANZO,NA WATU WENGI HAWALIONGEI HILI. WAANGALIE WANAMICHEZO WOTE WALIOACHA AU KUPUNGUZA MAZOEZI WANAVYOKUWA.
Refer Louis Nazario De Lima ( Ronaldo)
 
Mkuu nikifuata baadhi ya hayo mzoezi ndani ya mwezi mmoja nitakuwa nimepunguza kilo ngapi!?

 
Pole aisee!
lazima ufanye na dieting ama sivyo utazidi kunenepa
 
Haya mazoezi nimefanya sana lakini tumbo halikubali kuwa flat hata kidogo zaidi linakuwa gumu sana kwa ndani.
Unafanya kama hii routine niliyoionesha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…