Unataka upendwe vp we Gam...

Unataka upendwe vp we Gam...

Mtalingolo

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
2,181
Reaction score
410
"Ulilazwa hospitali miezi mitatu, Miezi sita masomoni yote nilivumili., Unataka upendwe vp Wewe Gam..*2, "

Maranyingi watu huwa hawakumbuki mazuri waliofanyiwa na wapenzi wao na mwisho wake huishia kuwasimanga na kuwaacha pasi na msaada wowote wala huruma juu yao pale wapatapo mafanikio...

Mtu umemvumilia wakati anaumwa miezi mitatu pamoja na kadhia zote za kukuhudumia mgonjwa kazivumilia,
Kavumilia miezi 6 ukiwa masomoni, kalea watoto wako au kutunza baadhi ya ndugu zako lakini baada yakupata mafanikio unamsahau na kutafuta mtu mwingine na kumuona yule hana hadhi tena...

Yatupasa tujue kuwa mambo hayo sio mazuri tu machoni kwa watu bali hata kwa mungu haipendezi kabisa...

Leo hii usaliti umekuwa mkubwa sio tu kwa wapenzi bali mpaka kwa wanandoa ambao kwa hiari yao walikula kiapo kwa imani zao kuwa watavumiliana kwenyeshida na raha lakin hali imekuwa tofauti kabisa...

Napenda kuiasa jamii juu ya suala hili la uaminifu na kwamba madhara yake nimakubwa sio tu kwa msalitiwa bali pia kwa msaliti, 1.Magonjwa mengi yameenea sikuhizi,
2.Vifo ambavyo hutokea baada ya kufumania/wa.
3. Na pia kuwekeana visa na chuki katika jamii..


JILINDE, JITUNZE, JITHAMINI,
2012 dunia yako, chaguo lako. Chagua kuwa mfano bora katika jamii...
 
Ni angalizo zuri ikiwa litazingatiwa kwa walengwa.
 
Ni angalizo zuri ikiwa litazingatiwa kwa walengwa.

walengwa ni wote ambao kwa namna moja au nyingine ni waathirika wa mambo tajwa hapo juu either kwa kutenda au kutendwa..
 
Back
Top Bottom