wanawake wote wenye watoto wanajua, mtoto lazima umuangalie kwa makini kinyesi chake.
huwa tunakisubiri kwa hamu sana kukiangalia kusaidia kurule out au kuthibitisha kuwa kuna tatizo. mara nyingine unaweza kumpeleka mtoto tu hospitali kwa sababu hujakielewa choo chake,
wengine huwakataza wafanyakazi kukitupa kabla hawajakiona hasa wakati unahisi mtoto anaumwa.
mie leo wanangu wakitaka kuniambia wanaumwa lazima wainclude katika maelezo yao mara ya mwisho kupoti, na ilikuwa aina gani. Na huyo mkubwa anajua tu kama anajisikia uchovu, hajapata bado, inabidi apate maji mwenyewe kwa wingi. Hata dawa (japo ni mpenzi) hataki mpaka maji yashindwe kazi.