Unauaga mwaka 2021 ukiwa ni mwaka wa aina gani kwako?

Ameen na ukawe mwaka wa heri🙏
 
Nilikaa jana nikautafakari kwa baadhi ya mambo ambayo nilijipa 100% kuyafanikisha huu mwaka lakini baada ya hapo nikajikuta nafyonza na kuinuka nilipokuwa nimekaa nikaenda zangu kulala.
 
Nilikaa jana nikautafakari kwa baadhi ya mambo ambayo nilijipa 100% kuyafanikisha huu mwaka lakini baada ya hapo nikajikuta nafyonza na kuinuka nilipokuwa nimekaa nikaenda zangu kulala.
[emoji16] ulifyonza yanini tukumbuke unapopanga Mungu nae anapanga.
 
Huu mwaka niliuanza vibaya sana. ulivyofika katikati nikaanza kupata mwanga fulani na mafanikio kadhaa.
Kuanzia mwezi wa 11 hadi 12 tarehe 10 mambo yalikuwa mazuri sana nikaanza kufikiria nitafute hata kiwanja niweke hata msingi, Hapa mwishoni mambo yamechenji huwezi amini.
yote kwa yote ninamshukuru mwenyezi mungu natumai 2022 utakuwa mwaka wa neema kwetu sote.
 
Ndio maisha mkuu tushukuru kwa yote.
 
Well i call it a year...Namshukuru Mungu kwa yote.. tusubiri 2022
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…