changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Leo Simba imetakata uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa ushindi mnono wa magoli matatu kwa sifuri.
Kocha wa Simba leo amemrejesha Aishi Manula katika kikosi cha kwanza na kufanikiwa kutoka na cleen sheet.
Kabla ya mechi hii kulikuwa na maneno mengi sana mitandaoni na pia washabiki walikuwa na jazba sana wanapo hojiwa kuhusu mwenendo wa Simba na wengi wakiwa wanalalamika juu ya uwezo wa kocha wa sasa wa Simba kuwa hana uwezo wowote ule, na kisha walionekana zaidi kumlilia kocha wa zamani, Patrick Ausems (Uchebe) kuwa uongozi umrejeshe tena msimbazi.
1. Je, kwa ushindi wa leo wa Simba dhidi ya Mtibwa mnasemaje kuhusu huyu kocha uwezo wake bado hana uwezo aondoke au ana staili kubakia Msimbazi?
2. Mashabiki wa Simba walipiga kelele nyingi sana kwamba Manula sio kipa ni shati tu hana uwezo wowote bora ya Kakolanya, hapo hapo wamesahau mema ya Manula ya kuwebeba mara nyingi sana kwenye kupangua one against one (ka-save clear chances).
Baada ya mechi ya Simba vs Yanga, Manula akaanza kuchomeshwa mahindi kwa kuwekwa benchi na nafasi yake kuchukuliwa Beno Kakolanya aliyepigiwa upatu na wanamsimbazi kwa vile Manula ni pazia.
Lakini tokea achezeshwe Kakolanya, katika mechi sita kaambilia clean sheet moja tu (Kama kumbukumbu zangu zitakuwa nimepuyanga mtaniweka sawa)
Pamoja na hayo yote hakuna aliyemfungulia uzi Kakolanya kuwa ni pazia utasikia makosa ya beki, lakini makosa hayo hayo yakiwa kwa beki na kipa akiwa Manula hutosikia akilaumiwa beki zaidi ya Manula ni shati sio goli kipa.
Je, ni kweli Kakolanya ni kipa mzuri kuliko Manula?
Karibu mtoe maoni yenu
#team uchebe #team kishingo #team Manula #team Kakolanya # team vigeugeu #washabiki na wapenzi wa Simba #wapenzi wa mpira wa miguu #wengineo