Unauonaje mwenendo wa klabu ya Simba kimchezo chini ya Kocha Sven Ludwig Vandenbroeck?

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151

Leo Simba imetakata uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa ushindi mnono wa magoli matatu kwa sifuri.

Kocha wa Simba leo amemrejesha Aishi Manula katika kikosi cha kwanza na kufanikiwa kutoka na cleen sheet.

Kabla ya mechi hii kulikuwa na maneno mengi sana mitandaoni na pia washabiki walikuwa na jazba sana wanapo hojiwa kuhusu mwenendo wa Simba na wengi wakiwa wanalalamika juu ya uwezo wa kocha wa sasa wa Simba kuwa hana uwezo wowote ule, na kisha walionekana zaidi kumlilia kocha wa zamani, Patrick Ausems (Uchebe) kuwa uongozi umrejeshe tena msimbazi.

1. Je, kwa ushindi wa leo wa Simba dhidi ya Mtibwa mnasemaje kuhusu huyu kocha uwezo wake bado hana uwezo aondoke au ana staili kubakia Msimbazi?

2. Mashabiki wa Simba walipiga kelele nyingi sana kwamba Manula sio kipa ni shati tu hana uwezo wowote bora ya Kakolanya, hapo hapo wamesahau mema ya Manula ya kuwebeba mara nyingi sana kwenye kupangua one against one (ka-save clear chances).

Baada ya mechi ya Simba vs Yanga, Manula akaanza kuchomeshwa mahindi kwa kuwekwa benchi na nafasi yake kuchukuliwa Beno Kakolanya aliyepigiwa upatu na wanamsimbazi kwa vile Manula ni pazia.

Lakini tokea achezeshwe Kakolanya, katika mechi sita kaambilia clean sheet moja tu (Kama kumbukumbu zangu zitakuwa nimepuyanga mtaniweka sawa)

Pamoja na hayo yote hakuna aliyemfungulia uzi Kakolanya kuwa ni pazia utasikia makosa ya beki, lakini makosa hayo hayo yakiwa kwa beki na kipa akiwa Manula hutosikia akilaumiwa beki zaidi ya Manula ni shati sio goli kipa.

Je, ni kweli Kakolanya ni kipa mzuri kuliko Manula?

Karibu mtoe maoni yenu

#team uchebe #team kishingo #team Manula #team Kakolanya # team vigeugeu #washabiki na wapenzi wa Simba #wapenzi wa mpira wa miguu #wengineo
 
Kocha hakukosolewa kwa mechi moja tu...alianza kuonekana hafai baada ya kuonesha uwezo hafifu kila mechi,anashinda kwa tabu, hatimaye akafungwa juzi. Ndo kelele zikawa nyingi.
So pia hatapongezwa ama kusema anatosha kwa game hii ya leo. Bado!! Kama ulikuwa upepo tutajuaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapima upepo wa kombe, ukimpepeta ndio kwaheri mwalimu!
 
Kwa maoni yangu leo Simba wamebebwa, Mtibwa wamenyimwa penati na yule kipa wa Mtibwa kapewa muhamala, haiwezekani Simba kufunga magoli matatu.

Alisikika mlevi mmoja akisema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kocha hatuwezi kumjaji kwa sasa iwe kumkosoa au kumsifia kwa hii mechi ya leo, nafikiri tumpe mechi kama 5 hivi ndo tunaweza kumjaji
 
kocha hatuwezi kumjaji kwa sasa iwe kumkosoa au kumsifia kwa hii mechi ya leo, nafikiri tumpe mechi kama 5 hivi ndo tunaweza kumjaji
Mashabiki hao hao waliomjaji Uchebe kuwa hafai kuifundisha Simba kisa tu amefungwa na mwadui kisha kutoa sare na Prisons. Na hao hao mashibiki wamepiga kelele kuwa Kishingo hafai kisa tu Simba kafungwa na Polisi Tanzania. Kwani mpaka mnafikia kumuona Kishingo hafai kashinda mechi ngapi na kupoteza mechi ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mashabiki wa soka bongo ni vigeugeu kupita maelezo... At least wa yanga kwa sasa wametulia,wasimba sasa shida sana.
 
kashinda mechi zaidi ya 5 na amepoteza mechi 1 tu dhidi ya JKT TZ
 
kashinda mechi zaidi ya 5 na amepoteza mechi 1 tu dhidi ya JKT TZ
Kwa takwimu hiyo, Mbona ana matokeo mazuri tu sasa kwanini kelele za hatumtaki kishingo zimekuwa nyingi sana baada ya Simba kupoteza mechi ya kwanza tu. Inamaana shida ni kutokuwa na uvumilivu kwa mashabiki au kweli hana uwezo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mashabiki wamekosa uvumilivu tu, wanataka washinde kila mechi bila kujua raha ya mpira mpira ni kufunga, kutoa suluhu na kufungwa ili kuongeza msisimko wa mpira
 
Uzuri wa sisi simba hatutaki ujinga hatutaki kusikia droo au kufungwa daima twataka ushindi
 
Kishingo asihukumiwe kwa mechi ya juzi, bado ziko mechi za kutosha.

Kishingo aendelee kuaminiwa!
 
Kiongozi unataka tumjadili kocha au kakolanya?
 
Hivi wanosema Sven kafungwa mechi moja waliangalia vizuri kweli mechi za Simba dhidi ya Mwadui, Namungo na Polisi? Je kweli zile mechi Simba ilishinda kihalali? Na Je pefomance ilikuwaje?

Watu wengi walikuwa wanamlalamikia kocha kwa sababu zifuatazo:-
1. Upangaji mbovu wa kikosi kama anapiga ramli badala ya kuangalia uwezo wa mchezaji na aina ya
ya wapinzani anaoenda kukutan nao. Kuna baadhi ya mechi alishindwa kabisa kupanga kikosi
sahihi.
2. Kutumia mshambuliaji mmoja badala ya wawili. Ikitokea mshambuliaji huyo kakamatwa vizuri na
mabeki wa timu pinzania na wakiwa na kiungo mkabaji mzuri basi mashambulizi yote yana hamia
katika lango la Simba muda wote wa mchezo.
3.Kushindwa kufanya "sub" kwa wakati sahihi na kwa mchezaji/wachezaji sahihi.
4. Timu kucheza "square pass" zaidi nyuma badala ya kupeleka mpira kwa haraka mbele kabla
wachezaji wa timu pinzani hawajajipanga.
5. Timu kukaba kwa macho

Ila kiukweli dhidi ya Mtibwa timu imerudi vizuri nadhani sasa Sven atakubali kuachana na falsafa yake aliyokua ameing'ang'ania ya kutumia mshambuliaji mmoja. Timu ilikaba kuanzia mbele, wachezaji walifika kwa adui kupambania mpira, viungo walipeleka mipira mbele kwa wakati na mabeki walipata kashi kashi kidogo hivyo ilipunguza sana madhaifu ya mabeki kuonekana. Mara ya mwisho Simba kucheza namna ile ni mechi ya duru la kwanza dhidi ya Kagera Sugar pale Kaitaba.

Ukweli lazima tuseme timu ikiboronga lazima tupige kelele kwani huko mtaani inabidi turudi usiku sana kuwakwepa mahasimu wetu. Na timu ikifanya vizuri lazima tuwapongeze. Kwa mechi dhidi ya Mtibwa Kocha na benchi lake la ufundi, wachezaji na viongozi wanastahili pongezi.
 
Kiongozi unataka tumjadili kocha au kakolanya?
Huoni kama kuna hoja mbili za kujadili? Moja kuhusu uwezo wa Sven kuendelea kuufundisha simba au bado asepe pamoja na Simba kuichakaza Mtibwa.

Hoja ya pili ni nani kipa bora zaidi ya mwenzie kati ya Kakolanya na Manula anayeweza kuisadia Simba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna aina ya ulalamikaji, kibaya zaidi viongozi wa timu hizi kariakoo wanasikiliza sana maneno ya mashabiki badala ya kufanya kazi zao kwa kuzingatia misimamo yao. Mashabiki walivyopiga kelele nyingi za hatumtaki uchebe na chupa wakamrushia kisa tu matokeo ya mechi moja kupoteza na sare moja kilichofuata ni kweli Uchebe kafungashwa virago.

Hivi sasa mashabiki waliona waliona ni kosa kubwa ulifanyika kumfukuza uchebe pasipo kukumbuka hisia na mihemko yao ndio yaliyopelekea hayo yote.

Kwahiyo kwa Sven, hayo matatizo hayo ulioanisha ni sahihi kwake kutimuliwa baada ya kufungwa na Polisi Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…