Saa inavaliwa kutokana na mkono mtu anaotumia sana. Kama mtu anatumia mkono wa kulia (Right Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kushoto. Na kama mtu anatumia mkono wa kushoto (Left Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kulia.
Hii inatokana na hatari ya kuivunja, kuiharibu au kuichakaza saa yake.
#Sio Lazima Kufuata Principle Hii.
Nimependa huu ifafanuzi,lakini ngoja nichangie.
Kuna ambao huvaa saa za chuma na kulegeza mkanda yaani saa inapwerepweta anaigeuza atakavyo(binafsi sipendi)haitulii pahala pamoja
Na mara nyingi hizi ni saa za chuma.
Watu wa aina hii kuepuka usumbufu wavae mkono ambao hauna harakati nyingi.
Kuna ambao huvaa saa hizo hizo za chuma au zingine za mipira, lakini mikanda yake mipana mno kiasi kwamba hata kuandika haandiki vizuri.
Mtu kama ana harakati nyingi za kuandika andika basi kuepusha usumbufu pia bora avae katika mkono ambao hatumii kufanyia shughuli zake.
Alafu kuna ambao huvaa saa za chuma lakini zimekamata vizuri mkononi kiasi kwamba hata ufanye harakati za kunyanyua mkono bado saa iko pale pale hawa wanaweza kuvaa katika mkono wao wa kulia kwa sababu saa haimsumbui wala kumtia uzito.
Lakini zipo saa za aina nyingi sana ambazo kwa watu wanaopenda kuvaa mkono wa kulia zipo saa nyingi tu ambazo haziwezi kuwasumbua endapo watavaa kwa mkono huo.
Saa mikanda membamba,nyepesi,inakaa vizuri mkononi,imebana vizuri japo sio sana,hizi saa zipo nyingi sana.
Lakini pia kuangalia kazi ya mtu ni muhimu sana.
Mfano kuna watu wao kazi yao kubwa ni kuandika ofisini labda wanatumia mkono wa kulia,mtu huyu pengine akaacha kuvaa mkono wa kulia kwa kudhani harakati nyingi zitaharibu saa yake,huyu anajinyima tu kwa sababu neno harakati linamtisha wakati hakuna harakati hiyo ya kutisha.
Neno harakati liangaliwe tena kwamba ni harakati zipi.
Kuandika ni harakati,kuuza bidhaa ni harakati,kubeba zege harakati,ukonda harakati n.k
Binafsi kitu kingine huwa ninachotizama ni urahisi wangu wa kuangalia saa naupata ukiwa mkono gani.
Mkono wa kulia nimezowea kuvaa saa na kufanyia vitu vingi hivyo hata nikivaa saa ni rahisi kwangu kuangalia saa luliko mkono wa kushoto.