SoC02 Unavyoweza kutumia mshahara wako kujikwamua kimaisha

SoC02 Unavyoweza kutumia mshahara wako kujikwamua kimaisha

Stories of Change - 2022 Competition

Taric Hiyari

Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
5
Reaction score
3
Wapo watu wanaowakejeli waajiriwa wanadai eti kama "Mtu asiye na Elimu anaweza kuosha Magari mtaani na akaweza kukuza kipato” kuna sababu gani ya kuishi Maisha magumu Kazini au Ofisini ?

Upo Ukweli wa namna Fulani katika kauli hii kwakua wafanyakazi wengi wanaishi Maisha ya Ukata, kazi yao Kubwa ni Kupambana kuhakikisha Mishahara inakutana, Katika Mazingira ya Namna hii inakua ni Vigumu kupiga hatua za Maana katika Maisha.

Ukweli huo hata hivyo hauondoi Umuhimu wa Kuajiriwa na kufanya kazi Chini ya Mtu Mwingine, Kila mtu ana Wito wake katika Maisha yake anayoishi, Wapo watu wanaoweza kufanya kazi bila ya Kuajiriwa, Kimsingi watu wa aina hii huwa wana Uwezo wa Kubuni vitu mbalimbali na kuweza kuendesha Maisha yao, Furaha yao ni kujitengenezea Ajira na Kujitegemea na Kutengeneza Ajira kwa Watu wengine

Lakini pia Wapo wenye Wito wa kuuza Ujuzi kwa watu wengine, Furaha yao ni kutumia Ujuzi walionao kutatua Matatizo ya Watu katika Jamii, Hawa ni kama Walimu, Madaktari, Mainjinia n:k Unapowashauri waache Kazi wakafanye Biashara nyingine Kimsingi unawanyang’anya thamani waliyonayo kwa Jamii kwa Kuzingatia kua hakuna wakati kila mtu atajiajiri…

"Kama Ulivyo Mwili sio kila Unachokula kitakupa Vile virutubisho Sahihi na muhimu Mwili unavyohitaji, Basi hata Mafanikio Hayategemei Kipato Kile Unachokipata”

Wapo wafanyakazi wanaofikiria Ugumu wa Maisha wanaokabiliana nao unasababishwa na Udogo wa Kipato wanachokipata, Wanasema "kama wangelipwa Mshara Mkubwa zaidi”, Basi Maisha yao yangelibadilika, Dhana hii Haina Ukweli kama nitakavyofafanua hapa Chini

Wapo watu wanaolipwa Mshahara Mkubwa lakini Haukutani na mshahara Unaofuata, Kinyume na hao wapo wafanyakazi wanaolipwa mshahara mdogo zaidi lakini wameweza kufanya Mambo makubwa katika Maisha yao achilia mbali nyongeza ya asilimia 23.3 ya Mshahara iliyoongezwa

Tofauti ya Makundi haya Mawili sio kipato bali Namna "WANAVYOTUMIA KILE WANACHOKIPATA”, Unapoelekeza kipato chako kwenye Matumizi ya kila siku yasiyokua na Faida ni Dhahiri Shahiri utahitaji kiasi kikubwa cha Fedha ili Ufanikiwe kuweka Akiba, kwakuwa siku zote Maisha yasiyolingana na kile unachokipata hayawezi kukutoa Kwenye Dimbwi la Umaskini, kwa Mfano : Mtu mwenye Mshahara wa Tsh Milioni moja kwa Mwezi anapoamua kuishi kwenye nyumba inayogharimu Tsh Laki mbili kwa Mwezi, akatumia Tsh tatu kuendeshea gari la Mkopo, Akatumia Tsh laki nne kulipa mkopo kila mwezi, Mtu huyu atakua anaishi Maisha yasiyolingana na Kipato Chake. Kwa nje Kijana huyu anaweza kuonekana "Mambo safi” anaheshimika kwasababu kwa haraka haraka Mafanikio yake yanaonekana

Anaendesha gari ya Mkopo, Anaishi Mitaa yenye hadhi, anapumzika kwenye Maeneo ya Gharama kubwa lakini katika hali halisi Mafanikio hayapo hivyo,

Tunasema Hana Mafanikio kwasababu Mbili

1. Kipato kinaishia kugharamia mahitaji yasiyo ya Msingi katika Maisha

2. Kipato hiko hakiwezi kutosha kuweka Akiba itakayowekezwa kwaajili ya kuzalisha

Mazingira haya yanaweza kumshawishi kukopa kwa Watu ( Mara nyingine kwa wenye kipato kama chake ) ili asukume Maisha yake, Matokeo yake ni kuendelea kujididimiza kwenye kifungo cha Madeni zaidi yatakayomnyima Amani, Pia katika Mazingira haya Inaweza kuwa rahisi kufanya Maamuzi ya kuacha kazi katika Jitihada za kutafuta kipato zaidi, lakini hata anapopata kazi nyingine Maisha yanaweza kuwa yale yale, kwasababu tatizo linaweza kuwa ni namna anavyotumia kile kidogo anachokipata

Kwa Kumalizia Zipo njia na Mbinu mbalimbali kwa mtu wa namna hii ambapo kama akiweza kuzitumia basi ataweza kujikwamua kutoka pale alipo na kufikia Mafanikio anayoyahitaji kutokana na kile kidogo anachokipata,

Kitu cha kwanza na Cha Msingi kabisa Tuhitaji kuwa na Elimu ya Msingi ya Fedha, ambayo pengine ni vigumu kuipata kupitia Mfumo rasmi, Fedha kwa kawaida inaongozwa kwa kanuni zake ukiziheshimu Unaweza kuimudu Fedha na ikakufuata, unapozivunja kanuni hizi unaweza kutumia Muda mrefu kuitumikia fedha, kinachoongoza kanuni hizi kwa Mujibu wa wataalamu wa Uchumi Binafsi ni "Nidhmu ya Fedha”, Bila kujali kiasi gani cha Fedha unachokipata kwa mwezi, Unahitaji Uwezo wa kutokukubali mtindo wako wa Maisha Ubadilishwe na Ongezeko lolote la kipato, Ukifanikiwa kuwa na Nidhamu hiyo kiasi Chochote cha Fedha kinaweza kukupa Usalama wa Kipato chako unachokipata,

Muhimu ni Kuzingatia kuweka Akiba kwa kuamua kutofanya matumizi yako ya kawaida kabla haujaweka Akiba, Unapopata Mshahara elekeza Asilimia Fulani kwenye Akiba na kinachobaki kingine Matumizi, Unapoweka Akiba kwa Mtindo huu ni Sawa na kujilipa ili Ufanye Mambo ya Maendeleo

Pia vile vile kupunguza matumizi ya kila siku kwa kujiruhusu kuishi Maisha ya kawaida kwa kipindi fulani cha Muda, Wafanyakazi Wengi hutamani kutetea hadhi za Ofisi wanazofanyia kazi kwa Kuishi Maisha ya Hadhi kubwa, Matokeo yake Wanajikuta Wakifanya Maamuzi yanayoweza kuwagharimu, Mfano kijana anapoanza Kazi anakua na Shauku ya kuendesha Gari ili kujenga hadhi fulani inayolingana na Kazi anayoifanya,

Anapopata Fursa ya Mkopo Kazini, kijana huyu ni lazima atakimbilia kwenda kununua gari mapema mno pasina kupepesa Macho, Changamoto ni kuwa matumizi ya Namna hii ya Mkopo yatamgharimu kwa Miaka kadhaa, Kwanza atalazimika kulipa mkopo na Riba yake kwa Muda Mrefu hali inayoweza kumfanya asiweze kufanya Chochote kile cha Maana kwa Miaka kadhaa, Maamuzi ya namna hii huchangia Umaskini kwa Wafanyakazi

La Muhimu kuliko yote ni kufikiria na kuamua kuwekeza kile unachokipata ili uweze kukuza na kuongeza kipato chako cha Ziada, Tumia Ujuzi wako kujiongeza kiujasiriamali, Maarifa na Ujuzi ni Mtaji Mkubwa mno, Usikae kumlilia Mwajiri wako akuongezee kipato JIONGEZE, Faida waliyonayo wafanyakazi wengi ni Mkopo, Tumia Fursa za Mkopo kwa Faida, Wekeza Unachopata badala ya kununua vitu visivyozalisha.

Hata hivyo haulazimiki kuacha Kazi ili Ukafanye Biashara, Unaweza Kufikiria Kufanya kazi kwa kushirikiana na Watu wanaofanya Biashara Tayari,

Ukiwekeza Hatua kwa hatua, Unaweza kupata Mafanikio Ukiwa Kazini kwakua kuna Mifano mingi ya Watu walioamua na wakapiga hatua kubwa Maishani mwao.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom