Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Je Kiswahili ni bidhaa? Kwa vipi Kiswahili kinaweza kuuzika?
Swala hili linaweza kuwa geni kwako hasa kama hujawahi kupata fursa yakutangamana kimazungumzo au maandishi ya manguli hawa walugha yakiswahili kuhusu ubidhaishaji wa Kiswahili, ambao ni prof, Clara Momanyi, Dkt Mahenge, Wallah bin wallah, nimewataja hawa kwakuwa hata mimi nilisikia mara kadhaa kutoka kwao na juhudi wanazozifanya ili kuhakikisha Kiswahili kinatunufaisha.
Kutokana na maendeleo makubwa ya kiteknolojia mamilioni ya watu hutumia internet kila siku nahiyo inaweza kuwa fursa yakupata soko la bidhaa hii ya lugha. Katika andiko hili tutajadili njia za kidigitali kadhaa unazoweza kukitumia Kiswahili kukunufaisha kiuchumi kama ifuatavyo:
Kuwa freelancer mtandaoni. Ipo mitandao mbalimbali unayoweza kujisajili kama mfanyaji kazi wakujitegemea, mitandao hiyo ni pamoja na freelancer, fiverr na upwork
Kuwa mfasiri wakujitegemea mtandaoni, unaweza kujisajili katika mitandao kama Upwork au fiverr kama mtoa huduma wa tafsiri kama unao ujuzi walugha nyingine yaziada ya kiataifa kama kingereza, kichina au kiarabu, kama huna ujuzi wa lugha nyingine niwakati wako wakuanza kujifunza sasa. Nunua kazi maarufu za fasihi katika mtandao wa amazoni nakisha uombe kuzitafsiri kwa lugha yakiswahili na urudie kuziuza mtandaoni zikiwa kwalugha yakiswahili. Pia unaweza kutafuta makampuni yanayohitaji huduma ya tafsiri katika mtambo wa google.
Kuwa mwandishi wakujitegemea mtandaoni, unaweza kujisajili katika mitandao tajwa katika ( i ) kma mwandikaji maudhui wakujitegemea (freelancer content creator) katika Nyanja flani na ukaanza kutafuta ama kutafutwa na wateja wanaohitaji huduma hiyo. Baadhi ya maudhui unayoweza kuandika nipamoja na yale yanayohusu, elimu, bima, afya, ya kieletroniki na mengineyo kadri utakavyojaliwa.
Andika vitabu Umeme (E-books) vya kufundishia lugha na uviuze katika mtandao kama Amazon kidle n.k, Maendeleo ya teknolojia ya uchapishaji binafsi yamekua sana, waandishi wachanga wanaweza kuchapisha kazi zao bila kutumia gharama yeyote kwa kupitia makampuni ya uchapishaji wa kidigitali kama vile Lulu, Amazoni, na mingineyo
Anzisha chaneli ya Youtube ya kufundishia lugha ya Kiswahili. Hii itakulipa kupitia program ya matangazo ya Google (google adsense) au kwa wewe kuweka matangazo ya makampuni mbalimbali utakayoomba. Tegemea kukutana na ushindani mkubwa ukifanya jambo hili hivyo hakikisha unaandaa maudhui bora, na chaneli inakaa katika ubora.
Tengeneza APP/program tumishi ya Game la lugha na kulipakia play store au app store. Nikuulize swali utajiskiaje pale unapojifunza kichina huku unacheza na kufurahia? Bila shaka niraha sana nihivyo hivyo hata wajifunzaji walugha ya Kiswahili watafurahia pale watakapocheza huku wakijifunza Kiswahili, unaweza kuwasiliana na programmer/ mwanaprogamia yeyote kwaajili ya jambo hili akakutengenezea . hakikisha ni mwaminifu. Utaweza kuiuza program hii kwa bei utakayoweka kwa kila atakayepakua mfano dala 1 kwa kila mpakuo/download au ikawa bure na ukalipwa kwa matangazo ya program ya Google (google admob)
Anzisha tovuti ya kufundishia lugha ya Kiswahili. Unaweza kufungua tovuti iakayofunza wageni au wenyeji lugha yakiswahili na ukatoza malipo kwao, au ukatoa huduma bure na ukalipwa kupitia makampuni mbalimbali ya matangazo utakayojiunga nayo. Muhimu katika tasnia ya matangazo ya kidigitali malipo hutegemea na idadi ya watembeleaji hivyo kadri utakavyokuwa na watembeleaji wengi ndivyo utaona mapato. Unaweza kutafututa wateja/ watembeleaji kwa kutumia mitandao ya kijamii au kulipia tovuti yako itangazwe kwa nchi utakayoichagua au duniani pote.
Mwisho unaweza kusoma au kutafuta maelezo zaidi kwa kutumia mitambo tafutishi ya mkondoni katika simu yako ya rununu au tarakilishi yako.

Upvote
26