Hamna kitu kama hicho. Ni fikra potofu.Mojawapo ya story huwa nazisikia sana na mtu kuwatoa watoto wake au ndugu zake kafara ili afanikiwe katika biashara au siasa. Utoaji kafara huwa unaelezewa kwa mtu huyo aliyoetolewa kafara kufariki kwa kinachodhaniwa kifo cha utata au kupatawa matatizo ya akili(kichaa).
Unaweza kuonyeshwa kichaa fulani ukaambiwa huu ni mtambo wa kutengeneza pesa wa tajiri fulani au ndio chanzo cha mafanikio cha mwanasiasa fulani.
Unajuaje au unathibitishaje kwamba fulani amefanikiwa kwa sababu ya kafara ya mtoto, mzazi, mke au ndugu yake?
Santa Claus yule anayeshukaga kwenye chimneys kushusha zawadi za watoto wakati wa Krismasi, yupo?Lisemwalo lipo! Hayo mambo yapo katika ulimwengu wa Giza!
Nadhani wenye taarifa kuhusu mambo hayo ni Mafundi yaani Waganga wa kienyeji.
IllusionYaani Umeamka Zako Usiku Unaenda Msalani Nje Ukutane Na Lijitu limepak mavitu meupe Usoni..halielewek..Unashangaa Nalo Limekukazia Macho utajiuliz Mara mbil mbil aliyeko mbele yangu Ni Nani?..
Kitu Kiliniacha Na Bumbuazi Hadi Leo.Yule Ni either alitaka antishe au dawa zake ziliisha Nguvu Sabab mm Sina Nguvu yoyote ya kumwona mchawi Na Nlikuwa Bado Dogo
Eleza jinsi Kazi ya kuchekesha inavyowezesha kupata utajiri wa Kujenga ghorofa. Otherwise ni kuwekwa loop ya kutafutwa kwa siri (?) Kuelekea kwenye utapeli?,Huyo mama ni tajiri kabla ya kugundua pesa zake ni za madawa nilienda kukaa likizo kwake.
Hilo jumba la kifahari nilijihisi mtoto wa mfalme nikapewa chumba ghorofani kipo full kuanzia tv mpaka friji.
Kuna watu wanaishi kama wapo mbele vilee halafu kazi yake anayoifanya nikisema inachekesha
Niishie hapa labda yupo humu asije akaona akaunga dots usiku akanifata buree
Ndio maana watu wengi waliofanikiwa wapenda kuwa na mitaa yao kuishi kiutulivu peke yao, hiyo mitaa hauwezi kukuta uswahili swahili wa kijinga.
Kuna ulazima gani haswa hadi Watu wote tuwe matajiri?Mbona wengi wanamuomba na wanafanya kazi kwa bidii na uaminifu sana ila bado wanakufa wakiwa masikini??
Hahahahaaaa..Ndugu yangu haya mabo yapo omba Mungu akuhepushilie mbali unaweza kutolewa kafara wewe..
Thibitisha neno utajiri lipo kwa nyanja gani na kwanini tusimuamini huyo uliyemnukuu ila tukuamini wewe.Ufalme wa mbinguni haupo.
Habari za ufalme wa mbinguni ni habari za kuwafariji maskini na umaskini wao.
Heaven is the promise for the poor so that they don't demand happiness on earth.
A poor man who has Jesus is richer than the rich man without Jesus. Hivi ndivyo maskini wanafarijiwa na umaskini wao kupitia imani za kidini.
Yani watu maskini choka mbaya wanafarijiwa kwamba watamiliki utajiri wa kutosha mbinguni, Hivyo wasijihangaishe sana kuwekeza duniani.
Utamu wa pesa uusotee si kupata pesa kirahisi rahisi tu, pia si wote tunaopenda maisha marahisi marahisi tu bila ya kuvuja jasho na damu.Kusubiri nini?
Kusubiri hadi lini?
Huyo Yesu hajui wajibu wake kwamba anapaswa kuwapa watu utajiri bila wao kuhangaika kumuomba kila siku?
Au huyo Yesu ni msahaulifu sana hadi akumbushwe kwa kuombwa?
Kuna walokole wamemuomba huyo Yesu miaka nenda rudi na hakuna chochote walichopata wakafa maskini na ukapuku wao.
Moja nyanja ya kuweza kumudu basic needs siku zote na wakati wote pasipo kuhitaji msaada.Thibitisha neno utajiri lipo kwa nyanja gani
Kwa sababu hayupo na hajawahi kuwepo.na kwanini tusimuamini huyo uliyemnukuu
Sihitaji uniamini mimi.ila tukuamini wewe.
Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Si wote, wewe na nani?Utamu wa pesa uusotee si kupata pesa kirahisi rahisi tu, pia si wote tunaopenda maisha marahisi marahisi tu bila ya kuvuja jasho na damu.
Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Huo msimu huyo chatu alipokuja haukuwa msimu wa neema kwa wakulima wengi? Kuna miaka Tanzania wakulima nchi nzima au baadhi ya maeneo wengi wao wanazalisha sana na miaka mazao yanakuwa haba, inawezekana ujio wa chatu uligogana na msimu wa neema kwa wakulima wengi nyie mkafiriki chatu ndiye anasababisha mzalishe sana mazao na mifugo.Yoda
Kwa sababu umeuliza wacha leo nikuambie visa3 sio vya kuhadisiwa
Kisa cha kwanza ni babu yangu mwenyewe. yeye ni mnyantuzu alienda kwa mganga akafanyiwa yake kisha akaapiwa nakuambiwa nenda baada ya siku kadhaa atakuja mgeni mpokee kwa ku nyunyizia maziwa fresh yaani yale maziwa unayameza mdomoni kisha unayapuliza ukimpulizia huyo mgeni na muda huo hujui mgeni atakuwa aina gani.
Babu akarudi kusubiri mgeni baada ya siku 9 mchana wanamenya mihogo kwa ajiri ya udaga chatu mkubwa wakamuona anakuja nyumbani family ikatahamalaki kwa uoga na wengine kufata fimbo.
Cha ajabu babu akaagiza yafatwe maziwa na kutekeleza kama aliyoambiwa baada ya kumaliza zoezi lile nyoka alienda moja kwa moja hadi sehemu ile ya kuhifadhia nafaka ninyi waswahili mnaita stoo huku kuna majina kama ng'hunguku ama kwenye maruli.
chatu yule alikuwa na tabia ya kwenda na kurudi akirudi mifugo itazaa sana yaani kila kazi ya mwanafamilia atakayofanya
inakuwa na mafanikio tele sio kilimo wala mifugo vyote vilienda vyema.
Kuna jamaa mwingine sitataja uhusiano wake hapa ila ni ndg kabisa. kazi yake ya kuchimba dhahabu huyu jamaa alikopa hela za kutosha bank na akashindwa kurejesha jamaa akawa katika msongo mkubwa wa mawazo.ndipo akaambiwa na jamaa yake wa karibu mchimbaji wa dhdhabu vilevile akampa abc zote na kumhakikisha swala lako ni dogo sana hili iwapo upo tyr twende kwa mtaalamu. kwa sababu ya umaarufu aliokuwa nao pia kufirisiwa anaogopa aliukubali ushauri wa jamaa.
Walipo enda akapewa maelekezo yote kisha akaombwa kijana wake wa kwanza . jama hakusita na dogo akapita kushoto. Basi ukwasi ukazidi mara2 zaidi ya mwanzo tena kwa ghafla mnoo duara zake zikawa za kugusa tu anapata. mfano mwaka 2017 yeye mfuko wa mawe ya duara zake kg50 alikuwa anauza m13 wengine m1au tatu wengini ni laki7 nk.
Nikiwa kama kiongozi wa duara zake tulikuwa tunafanya makubwa sana na tukiwa ofisini kwakwe kuna mambo ya kutisha tulikuwa tunaona watu 3 tu yaani mimi yeye na mtoto wake wengine hawaoni.
mfano siku moja nikiwa mwazwilo machimboni mimi na mtoto wake tulipewa maagizo na jamaa kuwa leo mnaugeni hapa mtafanya kama nilivyo waambia. tukakubali na tukasubiria huo ugeni uje midaa kama ya saa8 mchana tuliona mnyama wa ajabu maarufu sana Tz hii kaambana na chatu mkubwa mno. baada ya kuona tuliingia ndani kufanya yetu mkitoka kule ndani wa nje hawamuoni mtafanya kila kitu lakini kamwe hawatakuona hata awe mchawi hawezi kukuona. Yule mnyama alipofika kambini akiwa na chatu na wanatembea taaratibu tukafanya kama tulivyoambiwa na kuwaruhusu warudi. Na walikuwa wanaenda kupotelea maduarani wanaishia bila kuelewa wameenda wapi.
Kitakachofuata hapo ni duara zitachanganya hadi na ninyi mnachanganyikiwa pia hela nje nje.
Huyo jamaa akao mke wa2 na hapa sasa story ya kumtoa mtoto wake wa kwanza tuliijua yule mke mkubwa alienda akiria kwa mama mkwe wake akisema hadharani "'mama unajua kabisa nilimtoa mwanangu ili tufanikiwe kimaisha na mme wangu leo tumefanikiwa kaoa mwanamke mwingine Nimemoksea nini mimi mwanao?" kama haitoshi hapo nyumbani mtoto mwingine (KE) alikuwa na kichaa na yeye kumbe kashawekwa akianza anguka ama kutoka makamasi na kufanya mambo ya ajabu ajabu.Biashara za jamaa ndo zinapamba moto sana na aliyekuwa anasimamia ni huyu mwanamke wake mkubwa mtama akaumwaga wote ndo kujua kumbe mtoto alikufa kimaajabu ajabu kumbe sababu ilikuwa ni hii.
Mimi baada kutoka machimboni nikiwa na hela kiasi chake yale mambo japo niliya zoea lakini bado yalikuwa yana nisumbua sana kichwani hata nikiwa nimelala mara napiga yowe usiku maana yalikuwa yananijia mara kwa mara.
Nilikaa na wazazi nikaawaambia yote jibu la wazazi lilikuwa ni moja tu kutoka kwa mzee KAMA UNAJUA SISI NDO TULIOKUZAA ACHANA MARA MOJA NA NDG YAKO HUYU NAWEWE ATAKUPELEKA HUKOHUKO MWISHO UTUUE.muda huo mama akilia akisema ungeliwa na yule chatu nani angetuambia?
Ya3 sitaandika zitoshe hizi tu.
Mara zote huwa nasema hapa Iwapo unaamini kabisa haya mambo hayapo yamkini uko sawa kabisa.Na yule asiye amini kuwa yapo yupo sawa vilevile.
NIMESHAOKOKA SAII MSIJE PM. BWANA ASIFIWE SANA.
kwahiyo mama angekubali tusingekuwa na ephen_Mimi namjua mmoja alikua rafiki wa mama yangu utajiri wake ni wa kutumia nyota za wafanyakazi wake
Ila ilipofika mwaka 2018 ikabidi amtoe mtoto wake na akafanya hivyo
Ashawahi kumshawishi mama yangu ajiunge huko mama akakimbia nduki na urafiki ukaisha.
Alikuja dar kama housegirl kutoka Upareni ila sasa hivi ni tajiri.
kwanini RebecaKama mimi sijui nimetolewa kafara sijijui tu lol
Ningeshare lakini wacha nife nalo tu...kuna mtu anajiita Wagumu Tunadumu humu unamjua? Lolkwanini Rebeca
hebu share usije ukavuka nalo, huyo namuona ona tu, ndio aliyekutoa kafara?Ningeshare lakini wacha nife nalo tu...kuna mtu anajiita Wagumu Tunadumu humu unamjua? Lol
Hahaaaa hapana huyu mkuu jina lake nimelipenda, nataka niishi kwenye jina lake ...lol...mkuu tusiende mbali mimi kuweka reality yangu humu sitakaa kufanya hivyo, wanaonijua watakua wanajua naongelea masahibu gani...wasionijua basi bwana...hebu share usije ukavuka nalo, huyo namuona ona tu, ndio aliyekutoa kafara?
wengine hatukujui, hivyo hatutajua chochoteHahaaaa hapana huyu mkuu jina lake nimelipenda, nataka niishi kwenye jina lake ...lol...mkuu tusiende mbali mimi kuweka reality yangu humu sitakaa kufanya hivyo, wanaonijua watakua wanajua naongelea masahibu gani...wasionijua basi bwana...