Nakumbuka mzee, wakt nilikuwa standard three au four pale mpakani primary school, manzese dsm. Baazi ya wachezaji walikuwa hawa:
Beya Simmba
Mao Mkami
Hussein Masha
Paul Rwechungura
Madata Rubigisa
Deo Njoore
Rajabu Risasi
Wengi wa wachezaji walihamia simba ya dar. Je mnamkumbuka yule mtangazaji wa rtd aliyekuwa mwanza, utapenda akitangaza mechi ya pamba na simba au pamba na yanga.
Nimemkumbuka Nteze John Lungu naye alikuwa kwenye hiki kikosi
Kipaji cha ukweli.
Alikuwa RTC Kagera, akipiga kapelo kama alivyokuwa Manyika Petre wa Yanga.
Musimsahau Hussein Tindwa, aliekufa kiwanjani siku simba ilipocheza na Raccah Rovers ya Nigeria, hapo ilikuwa baada ya Simba kuipiga Mufulira Wandereres goli tano bila, kumbuka mechi ya mwanza iliochezwa uwanja wa taifa simba ilipigwa nne bila, huo ulikuwa ni mwaka 1978 sijui wangapi wanakumbuka hii