Unaweka nini samaki wabichi wasing'ang'anie kwenye kikaango?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Napenda samaki wabichi ila changamoto ni kuwakaanga jamani.

Mimi huwa naweka ngano, nachanganya ngano na maji nachovya samaki wabichi kisha nakaanga. Wanatoka vizuri sana na wanakuwa watamu mno.

Tupe mbinu yako na wewe.

 
Ngano ya nini best mafuta yatakapo pata moto vizuri samaki hawezi kung'anga'nia kwenye kingaango.
Oo asante nitajaribu huenda naweka mafuta yakiwa hayajachemka vizuri.
 
Vipi ulisagia na tangawizi humo?
 
Wala huna haja ya kuweka ngano. Mafuta yachemke vya kutosha halafu usiwai kiwageuza watameguka. Kaanga mpaka upande uive ndo ugeuze.
 
Wapakae samaki chumvi ya unga, kwisha mchezo.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…