SoC02 Unaweza kufanikiwa kupitia biashara ndogo ndogo, nifuatilie

SoC02 Unaweza kufanikiwa kupitia biashara ndogo ndogo, nifuatilie

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 26, 2017
Posts
25
Reaction score
48
Salama wapedwa?, nawasalimu, leo nataka kushea na ninyi machache kuhusiana na hizi biashara ndogo-ndogo, ila nitajikita sana katika biashara ya mahindi, naamini usipokata tamaa kusoma kuna maarifa lazima uyapokee mazima-mazima, naomba zima tv yako, radio yako nk, halafu nipe akili yako yote kwa dakika chache, naamini hutajutia. Si sawa eeeh? Haya twende pamoja-;

Miezi kadhaa imepita mwaka huu-huu 2022 nilitoka Mwadui nikaenda Maganzo kwa ajiri ya kuwasalimia wazee, (Ilikuwa ni jumapili) nilipofika nikakaa kwa siku tatu tu! Nikiwa pale Maganzo, ilipofika jioni nikawaaga wazee wangu na niksondoka kuelekea "Senta" (Mahala ambapo biashara nyingi zinafanyika na kuna mpishano mkubwa wa watu) na huu huwa ni utaratibu wangu kila ninapoenda sehemu ambayo ni ngeni kwangu, huwa nafanya hivi kupasoma mahala hapo "Wanaishi vipi?" Na kuna fursa gani" na je ni kifanya biashara ipi ita-take impakiti.

Yaani kifupi nikafanya survey. Nikiwa katika saveyi zangu nikakutana na bwana mmoja anayejishughulisha na biashara ya kuchoma mahindi (ilikuwa ni kama saa mbili hivi usiku) nikaagiza "hindi" na nikaanza kulitafuna, kumbuka lengo langu sio hindi ila nilitaka nimho-ji kiundani zaidi ili anifafanulie vizuri kuhusu biashara yake na fursa zilizopo mahala hao.

Mazungumzo yetu yalikuwa hivi:

MIMI: Kaka habari ya kazi?" Tafadhari naomba nichomee huu muhindi (Nikaugusa kabisa) nimeupenda.

MUUZAJI: "Poa kaka karibu sana (Huku akitabasamu) aaahaa unataka huu muhindi?", Usijali, subiri kama dakika kadhaa utakuwa tayari, karibu na bechi hili pembeni uketi.

MIMI; Ahsante, (Nikaketi) nikamuuliza, "Wewe ni mwenyeji wa hapa?"

MUUZAJI; Hapana-hapana (Huku akihudumia wateja na wakizidi kumiminika) mimi ni mwenyeji wa Kigoma hapa nipo kikazi tu, vipi wewe ni mwenyeji wa hapa?"

MIMI- "Ndio mimi ni mwenyeji hapa, japo sio saaaaana ila kwa sasa ninaishi Mwadui.

MUUZAJI - "Ok, sawa karibu sana."

MIMI: "Nashukuru. Nikataka nianze kumuhoji zaidi kuhusu biashara yake ya mahindi ila roho yangu ikasita kabisa, yaani "Imagine" mtu m-mekutana naye leo halafu unaanza kumuuliza faida anapata Tzs ngapi kwa siku" unadhani atakuchukuliaje?" Tena anaweza kukufukuza kabisa! Kwani uongo?"

NILICHOKIFANYA....

Baada ya kumaliza kula ule muhindi, nilimuaga vema halafu nikaongeza na muhindi mwingine halafu nikaondoka. (Ilikuwa ni kama mida ya saa tatu usiku). Kesho yake kama kawaida yangu nikamfuata pale-pale kijiweni kwake na nikaagiza muhindi na story zikawa zinaendelea tena akawa kaanza kunifahamu vema. Nikala muhindi halafu nikaondoka zangu mida ile-ile ya saa tatu.

Siku ya tatu tena jioni yake nikafika na nashukuru nilipoanza kuzungumza nae tu, akanitambua na akaniambia, "Karibu sana leo mangapi?" Nikamwambia, "Moja tu!" Naomba, akasema sawa na akaanza kulichoma huku akinichangamkia kwa furaha kubwa. Moyoni nikasema, "Hapa-hapa wacha sasa nimchomekee kuhusu hii biashara yake" basi, nikamuuliza kama ifuatavyo-:

MIMI-: "Ndio jamaa yangu mnasemaje hapa?"

MUUZAJI-: "Tupo tu tunapambana na maisha si unajua tena hakuna kupumzika"

MIMI- "Nikweli, halafu leo naona biashara inaenda vema sana, halafu unajua ukitafuna mahindi kiu kinakuja sana, kwanini usifanye utaratibu wa kuweka japo "Ka-kibanda" hapa hapa ka kuuza juice na maji?"

MUUZAJI - "Nina mawazo hayo japo mtaji ni changamoto kubwa kwangu, lakini natamani iwe hivyo"

MIMI- Kama una "Vision" hiyo hongera sana, ila mnapata sana faida hapa eee (Nikamchomekea)

MUUZAJI- "Tunashukuru Mungu mambo yanaenda vizuri tunapata-pata na biashara inazidi kusonga"

MIMI- "Hivi kwa siku unaweza kuuza mahindi mangapi?" (Nikafunguka kabisa baada ya kumuona kajaa)

MUUZAJI - "Inategemeana na siku lakini maximum hayapungui hamsini kwa siku ila kipindi cha gurio na nini hata mia na hamsini yanazidi"

MIMI- "Hongera unajitahidi mno-mno, pia mnayachukulia wapi?" (Niliogopa kumuuliza swali hili maana nilihisi anaweza hisi nataka kumuiga na kufanya biashara yake)

MUUZAJI - "Sana ni Sogwa (Kama kilometa 4 toka pale tulipokuwa tunaongea nae) lakini ikifikia kiangazi huwa tunaangaika sana kuyapata maana walimaji ni wachache.

MIMI - " Nikashusha pumzi (Maana nilihisi anaweza kunifokea kwa swali hilo) halafu nikamuuliza, "Je hindi moja wanawauziaje?"

MUUZAJI - "Akatabasamu halafu, akaniuliza vipi, wewe ni mfanyabiashara?" Halafu akaniambia kama ni masika huwa tunanunua mpaka hindi moja mia mbili (200/=) na mia hamsini. Na faida inapatikana ya kutosha.

MIMI - "Uko vizuri, kwa hiyo kwenye kila hindi unapata faida ya Tzs 300/= (Miatatu) si ndivyo?"

MUUZAJI - "Akatabasamu, halafu akaniambia, hapana inategemea na kiasi unachonunu, ukinunua mengi unaweza kupunguziwa zaidi."

MIMI - Basi moyoni nikawaza sana na nikapiga hesabu za kifanya-biashara fasta-fasta, nikawaza, amesema anauza mahindi zaidi ya hamsini kwa siku, inamaana kama kila hindi lina faida ya mia tatu-miatatu, mahindi hamsini (300×50= 15,000/=) kwa siku ni sawa na kiasi cha Tzs 15,000/= ambayo mara kwa mwezi 30×15,000/= ni sawa na Tzs 450,000/= mshahara wa muajiriwa wa serikarini kabisa, na hapo nimepigia idadi ya mahindi 50 tu, vipi akiuza mahindi 100, 150, daaah! Hawa jamaa wana hela sana aisee. Nikiwa naendelea kujiuliza.

MUUZAJI - "Kaka vipi nikuongeze lingine?" Au kwa leo umetosha?"

MIMI - Niongeze lingine (Basi akanipa na nikaendelea kulitafuna huku yeye akiendelea kuuza mahindi)

ALICHONICHOSHA ZAIDI NI HIKI...

Nikamuuliza jumapili huwa unafungua saa ngapi?" Akaniambia, baada ya ibada ya asubuhi huwa nakuja kufungua. Nikamuuliza, "Unasali dhehebu gani?" Akanitajia dhehebu lake na akaniambia ana mke na watoto na wote wanapata riziki kupitia hapo, akanigeukia akaniuliza, "vipi wewe je umeoa?" Nikamjibu, "Hapana bado" akaniambia, "Unasubiri nini?" Au mpaka maisha yakae vizuri?" Nikacheka halafu nikamwambia wakati ujafika, ukifika, "Nitakujuza tu". Baasi tukaachana nae nikaendelea na mambo mengine.

SASA MAJUZI..
Nikawa namshirikisha rafiki yangu mmoja hii habari yote, akaniambia, unamsemea huyo bwana, namfahamu ni "Mzee wa Kanisa" kanisa fulani, na amenunua kiwanja juzi-juzi hapa kikubwa tu kupitia hiyo kazi yake na ameanza ujenzi taratibu. Kifupi Yuko vizuri mno.

MOYONI NIKASEMA..
Kumbe hakuna kazi ambayo haina faida, sasa nikajiuliza, "Kama vijana wana vyeti vyao na kila siku wanalalamika hakuna ajira, kumbe kule vijijini kuna mtu wa la-saba C" kajichimbia zake na mtaji wake ni kama elfu hamsini tu, then kajitupia anachoma mahindi na anakula faida faida ya kutosha tena anamkimbilia mfanyakazi wa serikarini. Katika maisha kinachotakiwa sio ukubwa wa ma-vyeti nk, ila ni nia ya dhati ya kupambana zaidi kufika juu. Naomba nikutie moyo kijana, "Bado unaweza kufanikiwa hata kama ni kwa kuchoma maandazi, hata kama ni kwa kuuza njugu, hata kama ni kwa kuuza dengu, bado unaweza kuwa Great- Usikate tamaa tu, Mungu anathamini sana juhudi zako.

Thanks all.

Mwl Deus M.Ndololo.
 
Upvote 3
Life on the ground ni tofauti mzee! Naona hapo hujapiga hesabu za mkaa, usafiri wa hayo mahindi na baadhi yanayoharibika n.k.

Ila kwa kuwa Watz ni wazuri wa kuongea na motivational speakers kuliko uhalisia utapata watakaokusupport.

Ukitaka kujua unachokizungumza sio uhalisia na hujafikiria mbali jiulize kama ana kipato unachokisema kakosa vipi mtaji wa kuanzisha hicho kibanda cha juice na maji?
 
Life on the ground ni tofauti mzee! Naona hapo hujapiga hesabu za mkaa...
Rafiki, hakuna chenye faida kisichokosa changamoto, ndio maana nimesema kuwa, katika biashara yake ya kuuza mahindi hasa siku za gulio anauza zaidi ya mahindi 150, hivyo tukapiga kwa kiwango cha kawaida cha mahindi 50 per day.

Ukweli ni kwamba nataka udake mema kutoka kwake na yale ambayo unaona yanaweza kuzuia mafanikio yake ndio uyafanyie kazi ili na wewe katika safari yako ya kibiashara uweze kufika mbali zaidi.

Huyu bwana, kama hatazuiwa na changamoto , zozote zile na akaamua kupambana kisawasawa nakuhakikishia baada ya muda kadhaa atakuwa mbali mno. Pia, eneo analofanyia biashara sio eneo lake ila kakodi tu hivyo mpaka ninavyozungumza na wewe leo, tayari mwenye eneo anaprocess za kufungua kijiwe cha kuuza juice na maji na yule bwana anauza mahindi kama kawaida.

Thanks kwa maoni yako.
 
Je? Na ww unafanya ipi bznes
Salama,

Nafanya biashara, nimeweka mzigo bank, na pia ninanunua na kuuza nafaka (Hilo sio muhimu sana) ila Ukubwa au udogo wa ninachofanya hakitakusaidia chochote kile kama hutopokea maarifa haya. Nataka uyameze hivyo-hivyo hata kama inakuuma.

Thanks.
 
Back
Top Bottom