SoC01 Unaweza kufanya hicho unachokitamani kifanyike ila fumbia macho hicho unachoona ni kikwazo kwako

SoC01 Unaweza kufanya hicho unachokitamani kifanyike ila fumbia macho hicho unachoona ni kikwazo kwako

Stories of Change - 2021 Competition

Rozney

New Member
Joined
Sep 11, 2021
Posts
3
Reaction score
3
UNAWEZA KUFANYA HICHO UNACHOKITAMANI KIFANYIKE ILA FUMBIA MACHO HICHO UNACHOONA NI KIKWAZO KWAKO.

Watu wengi wamekuwa wakitamani kufanya vitu vikubwa na vizuri na pia huenda ni vipya lakini wanakata tamaa baada ya kutazama maumbile, umri, kabila, jinsia na hata hali ya kimaisha na mwisho huishia kutamka neno "MIMI SIWEZI LABDA NINGEKUWA HIVI AU NINGEKUWA VILE"
Waswahili walisema"uoga wako ndio umasikini wako"

Tambua kuwa vile ulivyo ndio style ya pekee na yenye kuvuta mtazamo mkubwa wa watu na kushangaa kuwa umewezaje. Mfano wewe ni mlemavu unatamani kuonyesha ulimwengu jinsi ambavyo unaweza kufanya kitu flani kama mtu mwingine mwenye viungo Sawa, mfano kula kwa kutumia mguu badala ya mkono, unaweza kuimba, unaweza kutunga vitabu, usiangalie watunzi wenzako vile Wana ukamilifu wa viungo, usitazame kuwa wenzako wengi wanafanya kazi unayoitamani kuwa ni jinsia tofauti na yako, usitazame kipaji ulichonacho eti kinafanywa na watu wenye umri tofauti na wako na ukaishia kusema "MIMI NIMEPITWA NA WAKATI NIACHIE VIJANA"

Kama ni jambo lisilo na limit ya Muda unatamani kufanya, Anza sasa,

Usijiulize utaanza vipi? anzia mahali ambapo unapaweza kufanya, usisubiri uwe na pesa nyingi, anza na kile ambacho unacho kwani Sio kila kitu kinahitaji Msingi wa pesa, kuna vingine unahitajika uthubutu wako tu mfano kama una kipaji cha kuimba rekodi clip fupi tuma mtandaoni, ni hatua mojawapo ya kuanza safari ya mziki huwezi jua clip ile italeta matokeo gani, kuna watu wengi wamepata udhamini kupitia clip zao ambazo walizirusha kama utani na sasa wamesajiliwa kwenye magroup makubwa mfano msanii Angela ambaye amesajiliwa Kondegang.

Kumekuwa na mifano Hai ya watu ambao walifukuza mawazo ya kushindwa vichwani mwao na kukaribisha Neno NAWEZA, jinsi walivyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliko hata hao waliojulikana kuwa ndio wenye sifa kwa mfano zamani hakukuwa na waimbaji watoto wadogo,wazazi wengi waliona kuwa Sanaa ni uhuni, Hivyo watoto waliishia kusoma masomo ambayo walilazimishiwa na wazazi, na watoto walisoma ili tu kuwaridhisha Ila vichwani waliwaza kucheza mpira, kuimba kuwa wanamitindo, n. K

Kitu hiki kimefanya familia nyingi kuwa na migogoro kati ya wazazi na watoto wakibaki kulaumiana, mzazi akijutia kupoteza pesa kumsomesha mwanaye awe daktari lakini badala yake akaishia kukimbia riadha, kuimba, n.k.

Nchi zilizoendelea wameweza kipaumbele vipaji vya watoto zaidi kuliko kusoma ili waajiriwe na ndio maana bado kiuchumi wanatuacha mbali sana, watoto wa kichina tangu wadogo wanafundishwa vitu ambavyo inaonekana wanapenda na kuviweza na bidhaa nyingi ambazo watoto wetu wanachezea zinatengenezwa na watoto wa kichina katika kujifunza kutengeneza ndege, magari n.k,watoto wetu wanaletewa kucheza na kikiharibika hawawezi hata kurudishiwa vile kilikuwa.Nchi yetu tumeonekana kama ni dampo la kutupa bidhaa ambazo kule zilipotoka hazina Thamani.

Hii natamani ifikie mahali tuseme No, nasi tuwe na watu wenye kutengeneza vitu na kuuza nchi zingine.

Nchi yetu ya Tanzania haijawekea mkazo kuendeleza vipaji vya watoto wanasisitiza kusoma tu na Elimu yetu inategemea kuajiliwa, maelfu ya wasomi wanamaliza na kukosa kazi, baadaye baada ya Maisha kuwachapa mtaani, ndipo wanakumbuka kutumia vipaji ambavyo wanavyo na inakuwa ni too late kwani ni vipaji visivyo na uzoefu, wanaishia kushika nafasi za mwisho mwisho kwani Kuna watu wenye uzoefu wa muda mrefu. Ushauri wangu ni kuwa kuwe na mtaala wa kusoma masomo na vipaji pia, ili kuwe na plan A n B katika Maisha ya wasomi wa kesho.

Tukirudi kwenye point yetu, tunaona jinsi ambavyo wazazi wengi wameanza kuthamini vipaji vya watoto wao,

Sie wote ni mashahidi kuwa siku hizi Maisha yamebadilika sana Sio kama zamani ambapo hakukuwa na comedian watoto wadogo, hakukuwa na wasanii wa kike wenye watoto hata kama walikuwa nao, ila ilikuwa ni siri kubwa maana ingeonekana hana sifa za kuwa msanii hasa wa kuimba, ila nyie wenyewe ni mashuhuda wa kipindi cha Hivi Karibuni Kumekuwa na wimbi la wasanii wengi tena wenye majina makubwa kupata ujauzito na kuzaa watoto, mimba kwa wasanii wa sasa Sio siri tena ni jambo la kujivunia kuitwa Mama,japo Roseney nawapa ushauri kuzaa ndani ya ndoa, kwani pamoja na kusema kuwa, pamoja na kufanya Sanaa na Maisha ya kawaida inafaa yaendelee Ila inafaa tuangalie na kile ambacho tunafanya je tupo sahihi?

Natamani kuona kukiwa na mapinduzi makubwa ya fikra kuhusu kufanya jambo lolote wakati wowote bila kuwa na vikwazo, mfano mtu yoyote aliyeoa au kuolewa, aliyezaa au aliye na umri wowote kuonyesha kipaji chake bila shida, pamoja na watu wengi sasa Hivi kuwa na watoto huku wakiendelea na vipaji vyao bado suala la kuoa au kuolewa halijawekwa wazi, ni rahisi mtu kuonyesha jamii kuwa ana mtoto na si kuonyesha yule aliyezaa naye mtoto, au ni rahisi kuvalishana Pete ya uchumba kuliko kuvalishana Pete ya ndoa, Kwanini naongelea mambo haya, ni kwa sababu natamani tufikie mahali tuweze kufanya jambo lolote, wakati wowote bila kipingamizi chochote Yaani namaanisha mtu mwenye kipaji chochote aweze kukionyesha bila kujali, amezaa, ameoa au kuolewa, ana ulemavu, umri ni mdogo wala mkubwa.

Wasanii wengi Hivi Karibuni wamejifunza kwa Zari the boss lady ambaye ni X na mzazi mwenzake na msanii Diamond Platinum baada ya kutangazia umma kuwa ana watoto wakubwa na bado ni mrembo, mwenye pesa na anayeheshimika mahali popote.

Mama Huyu licha ya umri wake na hata umri na idadi ya watoto watano alionao lakini ukimwangalia ni kama hana hata mtoto mmoja, bado ni mrembo na mchakarikaji, wasichana na wamama wengi wamejiamini kuwa licha ya kuzaa bado wanaweza timiza ndoto zao.

Hivyo
Mfano huu unaonyesha dhahiri kuwa hicho Unachoona ni KIKWAZO wenzio wanajiamini na kufanya vitu vikubwa na jamii inawapa Heshima kwa sababu tu ya kujiamini. Kuna mifano mingi sana mtaani kwetu ambao hata wewe utakuwa na rafiki zako ambao wanajiamini lakini watu wengine wanawabeza kwa mionekano yao lakini hawajali na kila siku tunaona mafanikio yao.

Kuna wasanii na viongozi wakubwa duniani wenye ulemavu wa viungo, ulemavu wa ngozi,kuna wazee wenye pesa ambazo zimetokana na kufanya vitu mbalimbali na kupata mafanikio makubwa mpaka yakaishangaza dunia na jamii inayoizunguka.

Kitu kikubwa ninachokiongelea hapa ni Kujiamini, kuthubutu kufanya kile unachokiamini unakiweza bila kuangalia watu wanakuonaje, ili mradi kisivunje sheria za nchi na za dini.

Siongelei tu katika vipaji Ila kama Kuna wasomi wenye ndoto kubwa za urubani, udaktari bingwa na hata uongozi ngazi za juu bado inawezekana, jiamini thubutu usijione hufai kuendesha ndege kwa sababu ya ulemavu wala usione huwezi kuwa Rais kwa sababu ni mwanamke, fikra hizo futa kwani zimepitwa na wakati.

Watu wengi wanakwama katika uthubutu, mfano anaogopa kuanza biashara akiogopa kupata hasara, anaogopa kukopa akiogopa kufungwa pale akishindwa kulipa, anaogopa kuingia kwenye Mahusiano akiogopa kusalitiwa, Ondoa mawazo hasi kichwani yatakufanya ufe maskini, kila jambo linachangamoto lakini haimaanishi tuzikimbie

Nina imani baada tu ya kumaliza kusoma Maneno haya utajitathmini kufanya kile ambacho kimekuwa ni ndoto ya Maisha yako,bila kujali nani anasema nini, ukiamua kuanza safari usitazame mbwa wanaokubwekea utaghairi unapokwenda.

NAKUTAKIA SAFARI NJEMA KUELEKEA NDOTO ZAKO.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom