Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Kama kuhamisha kabila toka kwenye asili yao kuwapeleka sehemu isiyo asili yao ni jambo linalowezekana je, katika muktadha huo na mantiki hiyo unaweza kuwahamisha Wazanaki toka Butiama kuwapeleka Igunga inayopata wastani wa mvua 22-27mm (sehemu kame zaidi JMT) kwa mwaka?
Kama haiwezekani kwa Wazanaki mbona imewezekana kwa Wamaasai kupelekwa Handeni? Mizania ikoje hapa?
Tume ya Jiji la Dsm ilipitisha sheria ya kutaka wasio wazawa wa Dsm wanaponunua viwanja, mapagala na mbavu-za-mbwa katikati ya Jiji kuhakikisha wanapojenga majumba wasiwaondoe wazawa (wazaramo, wadengereko na wamanyema) bali wawape sehemu katika hayo majumba ili kuhifadhi historia yao hapo isipotee.
Kwanini hili lisingewezekana kwa Wamaasai wa Ngorongoro na Loliondo? Hii ya Wamaasai siyo ethnic profiling kweli?