Unaweza kuhisi umekumbana na lile gonjwa.

Unaweza kuhisi umekumbana na lile gonjwa.

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Ushawahi kuumwa homa za mara kwa mara, na kila unapokwenda hospitali kupima malaria, typhoid, UTI, n.k unaambiwa huna, unapewa dawa za kuondoa homa. Baada ya kipindi fulani unajikuta mwili haueleweki unarudi tena hospitali.

Hapo sasa unaweza kudhani kuwa tayari ushakumbana na lile gonjwa. Hey! wakati mwingine huenda unaumwa mara kwa mara kwasababu zifuatazo;

1. Kutofuata maelekezo ya dawa (daktari) - Kuna watu hawapendi kufuata maelezo ya dawa (daktari). Kwa mfano ameandikiwa kunywa dawa kwa siku mara tatu, lakini yeye ataruka maelekezo. Leo akinywa kesho hanywi, au akinywa asubuhi, mchana hanywi.

2. Kutokuwa na muda wa kupumzika - Dawa nyingine zinamtaka mgonjwa apumzike. Daktari akikwambia pumzika basi upumzike kweli, acha kubeba magunia wakati upo kwenye dozi.

3. Kutomaliza dozi yako - Kuna watu wengine wakipewa dawa za kuondoa homa baada ya "siku mbili tatu" wakijihisi wamepona wanaacha kunywa dawa. Wanatupa dawa jalalani kisha wanaendelea na mizunguko ya maisha ya kukimbizana Kariakoo.

4. Kutofanya mazoezi ya mwili - Kwa mfano mazoezi mepesi ya kukimbia, kuruka kamba, na mazoezi mengine. Mazoezi mepesi yatakusaidia kuuweka mwili wako vizuri pindi unaendelea kunywa dozi.

NB: Wewe huna lile gonjwa, ni uzembe wako wa kutofuata maelekezo ya daktari.

RIGHT MARKER
Dar es salaam
 
Back
Top Bottom