Unaweza kuingia mkataba wa milioni 50 Kwa kutumia business name?

Unaweza kuingia mkataba wa milioni 50 Kwa kutumia business name?

Kwa mfano nimesajili business name nataka kuchukua tenda ya kusupply Vitabu shule za msingi ,amount tendered mil 50, nitakuwa na capacity ya kuomba hiyo bid?
 
Hakuna lisilowezekana kwake yeye aaminiye.
 
Vicin nahitaji legal answer ,that's why nimeuliza humu
 
Kwa mfano nimesajili business name nataka kuchukua tenda ya kusupply Vitabu shule za msingi ,amount tendered mil 50, nitakuwa na capacity ya kuomba hiyo bid?
Umesajili Wapi? kama inafanya kazi kama kampuni unaweza vizuri tu
 
Vicin nahitaji legal answer ,that's why nimeuliza humu
Najua.
Ningekuwa na vifungu vya sheria ningekupa. Mimi nimekupa kile nilichonacho kutoka kitabu cha Marko.
 
Suala la kusajili jina la biashara halina uhusiano na wewe kupata tender. Jina la biashara hutambulisha biashara haswaa ila halikufanyi wewe kuwa kampuni, hadhi yako itabaki kuwa 'sole proprietor' labda kama utasajili kampuni.

Kila tenda ina vigezo na masharti mfano, inaweza takiwa muombaji awe na kampuni yenye mtaji wa uendeshaji (working capital) mathalani milioni 40 n.k sasa kitakachokupa tenda ni wewe kukidhi matakwa ya zabuni/tender hiyo wala si business name.
 
Back
Top Bottom