Unaweza kujifunza kitu kupitia mimi

Unaweza kuanza hata na laki mbili cha muhimu ni focus focus focus

Tusizarau biashara ndogondogo kutafutia mtaji.
Pia tusiwe watumwa wa macho ya watu oooh nikifanya biashara hii watu watanionaje!. Angalia nini lengo lako kwa wakati huo,na unacho fanya kweli ni njia ya kufikia lengo lako?
Biashara ina uwanja mpana hata mimi na wewe tunaweza fanya biashara zinazo fanana ila changamoto tutakazo pitia haziwezi kuwa sawa , kwahiyo hatuwezi kuwa na njia moja ya namna ya kutatua changamoto tutakazo kutana nazo.
Hapo ndipo ilipo tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine.
Ila mimi naamini ktk kuto kukata tamaa maana utajifunza mengi ktk kujisahihi kwenye makosa unayo kosea hatua kwa hatua mpka unakuwa bora kwenye kile unacho kifanya.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 


Hapa wengi sana ndo wamefeli!kuchagua biashara
 
Hongera kaka
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changamoto anayokutana nayo muuza mahindi keko ni tofauti na muuza mahindi wa tegeta kwa ndevu
 
I Wish Ningesoma Uzi Huu Nikiwa Na Mdogo Wangu Ila Lazima nimtumie link....Asante mleta mada.
 
Not: Nime anza kujitegemea baada ya kumaliza form, ninacho kumbuka baada tu kumaliza form four nililudi nyumbani ( kijijini kwetu )nikaomba mtaji ili niweze kuzufanya biashara.
Nilipewa mpunga debe3( ndoo 20ltrs 3) nakumbuka baada ya kuuza nilipata kama sh 23,000/= na ndiyo mtaji nilio anza nao mpka wakati natakiwa kwenda shule form five nilikuwa na cash zaidi ya 1ml. Ambayo nili itumia kama ada na matumizi mengine mpka nilipo maliza form six. Pia sikuwa nime imaliza kwakuwa nilikuwa mwangalifu sana ktk matumizi,lengo nibaki na mtaji uje kunisaidia tena baada ya kumaliza form six, ila bahati mbaya nilipo anza biashara kuna bwana niliye mwamini alitoweka(alikimbia) na mtaji wangu wote na kuniacha nikiwa sina hata pa kuanzia ndipo ikanibidi nitafute kazi ili nipate mtaji.
Unaweza takakujua ni biashara gani nili ifanya baada ya kumaliza form four kwa mtaji wa sh 23,000/=?
Biashara niliyokuwa naifanya ni kutafuta kuku vijijni kwa kulipa cash au kubadilisha na bidhaa na kwenda kuwa uza kwenye mji ulio kuwa karibu.
changamoto kubwa ilikuwa soko,nilimfata mama mmoja alikuwa na hotel yenye jina kwenye maeneo yale nikamuomba sana awe mteja wa kununua kuku wangu, mama alikubali na pia umri wangu Mdogo pia ulichangia mama yule kunionea huruma na kukubali kirahisi kufanya biashara na mimi. Namshukuru sana yule mama alinisaidia sana kukuza mtaji kwakua alinihakikishia soko la uhakika la kuku wangu.
Kazi haikuwa rahisi maaana mazingira yalikuwa magu ni vijijni misitu na sehemu nyingi unatembea kwa miguu hakukuwa na miundo mbinu hata kupita na baiskeli,na pia nakumbuka sikuwahi pumzika kuanzia mwezi 11 mpka mwezi 7 naenda kuanza form five.
KWA LEO NITAISHIA HAPA
NIKIPATA MUDA NITAENDELEA KUANDIKA ZAIDI.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Asanteni kwa kunitia moyo nikipata muda nita malizia sehemu nilizo katisha .
Naamini kunachakujifunza ndugu zangu

Ni kweli ndugu yangu uliamua kushikilia lengo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 


Haya wale mnaosemaga kwenye biashara kuna siri nyingi..oh ukiona mtu amefanikiwa ana siri nyingi sana hawez share na mtu.haya kujeni hapa!...jamaa kashare hapa kila kitu..ishu ni discpline ktka hela tu!
 



Mbona kama stori zinagongana...?hapo awali ulisema ulikosa ada kwa muda mrefu sana, ukachelewa kwenda shule, leo ada ulitafuta mweyewe na ukawa na zaidi ya 1M. yaani unataka kuniambia kuwa hii stori ni chai?
 
Haya wale mnaosemaga kwenye biashara kuna siri nyingi..oh ukiona mtu amefanikiwa ana siri nyingi sana hawez share na mtu.haya kujeni hapa!...jamaa kashare hapa kila kitu..ishu ni discpline ktka hela tu!


Hapa siamini sana,mazingira ya kijijini uanze mtaji wa shilingi elfu 23, utake na zaidi ya 1M...thubutuuuuuu kwa miezi kadhaa tu, kila mtu angekuwa na pesa bana.
 
Mbona kama stori zinagongana...?hapo awali ulisema ulikosa ada kwa muda mrefu sana, ukachelewa kwenda shule, leo ada ulitafuta mweyewe na ukawa na zaidi ya 1M. yaani unataka kuniambia kuwa hii stori ni chai?

Hayo ni Maelezo niliyo yafupisha ila hapa nime jaribu kufafanua kidogo .
Kueleza ni biashara gani pengine nilifanya.
Pia kuna changamoto zilikuepo siwezi kueleza kila kitu maana nashindwa hata kupangilia ila kulikuja mazingira ya kutaka kuzurumiwa nayo yalinipotezea muda, nili hama kutoka Pugu kwenda Tosamaganga mpka nalipoti shule wenzangu wana ludi midterm.
Not:mimi siyo mwandishi mzuri na pia kupata muda wa kuandika na kupangilia ili wenzangu wa elewe inanipa shida. pengine kwa kusimulia ina urahisi




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…